NA MADINA ISSA

CHAMA cha Demokrasia Makini, (CHADEMA) kimetangaza kusimamisha wagombea wa nafasi za Ubunge, Udiwani na Uwakilishi, katika Majimbo mbali mbali ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Chama hicho, Suleiman Faki Khatib, baada ya kujiunga na chama hicho kutoka CUF, huko Ofisini kwao Kisiwandui Mjini Unguja.

 Alisema kwa nafasi ya Ubunge Unguja wamewateuwa wagombea 16 ikiwemo, Kikwajuni, Welezo, Mahonda, Paje, Chumbuni, Nungwi, Malindi, Pangawe,  Mkwajuni, Amani, Mpendae, Makunduchi, Mwera, Tunguu, Mwanakwerekwe na Uzini.

Nafasi ya Uwakilishi majimbo yaliyoteuliwa alisema ni Kikwajuni, Mpendae, Chumbuni, Malindi,Mtoni, Dimani, Bumbwini, Makunduchi,Tunguu, Nungwi, na Mahonda

Upande wa Ubunge kutoka Pemba, majimbo yaliyoteuliwa wawakilishi wao alisema ni Gando, Mtambile, Konde, Ole, Pandani, Chakechake, Wete, Wawi, Mkoani, Kojani, Tumbe, Wingi, Mtambwe pamoja na Chambani.

Alisema nafasi ya uwakilishi majimbo yaliyoteuliwa ni Kojani, Gando, Pangani, Konde, Wawi, Ziwani, Mtambile, Mkoani, Wete na Chakechake. Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni wa Chama hicho Zanzibar, Kado Salmini Mwalimu, alisema wanakusudia kutoa kadi kwa wanachama waliojiunga na chama hicho.