WAKATI Samuel Lawrance raia wa Nigeria alipowasili nchini Japan akiwa na umri wa miaka17, maisha katika nchi hiyo yalikuwa magumu sana na matatizo ya lugha na utamaduni wa wajapan ulizidisha ugumu wa maisha.

Akiwa na umri wa miaka 34, Samuel sasa ni mhandisi mwenye mafanikio anayeishi jiji la Tokyo na anaelezea jinsi alivyokabiliana na ubaguzi akiwa skuli, chuo kikuu vitu ambavyo vimechangia kufikia nafasi aliyonayo hivi sasa.

“Nilipokuwa kijana balehe, nilipitia hali ngumu sana, kama vile watu kukwepa kukaa karibu na mimi katika treni, kwa hiyo kila mara kulikua na kiti kitupu karibu yangu lakini hakuna yeyote aliyetaka kukaa na mimi. Watu waliona afadhali wasimame ndani ya treni wakiwemo wazee kuliko kunikaribia. Nilijihisi vibaya sana nilitamani nisimame ili watu waweze kukaa”, alisema,

Samuel alisema anaamini Japan imekuwa na mabadiliko kidogo na sasa limekua taifa linalowatambua watu wengine, ingawa hali za ubaguzi katika treni bado linaendelea kujitokeza ingawaje mara chache.

Hakuna makadirio ya idadi ya watu weusi nchini Japan, kwani ofisi ya takwimu ya nchi hiyo huchukua data kwa utaifa, lakini wageni kwa ujumla nchini humo asilimia 1.7 ya idadi ya watu wa nchi hiyo.

Mnamo mwaka 2015, wakati mwanamitindo Ariana Miyamoto, binti aliyezaliwa na mama mjapani na baba Mmarekani mweusi, aliposhinda tuzo ya urembo wa ‘Miss Universe Japan’, suala la ubaguzi lilijadiliwa baada ya watu kumkosoa kutokana na rangi yake.

Ingawa Ariana alizaliwa na kulelewa nchini Japani, alishambuliwa kwa maneno na watu waliosema kuwa hakuwa mjapani vya kutosha na hivyo hakuiwakilisha nchi.

Mwezi Januari 2019, tatizo jingine la ubaguzi wa rangi lilijadiliwa. Mchezaji wa tenisi kutoka nchini humo Naomi Osaka alioneshwa akiwa na ngozi nyeupe katika kibonzo cha matangazo cha kampuni Nissin company, inayotengeneza tambi kinyume na muonekano wake. Jambo hilo lilizua gumzo, na baadae kampuni ikaomba msamaha kwa kitendo hicho.

Kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd, ambaye alikufa baada ya polisi mzungu kushindilia goti kwenye shingo yake, kiliibua wimbi la maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi mwezi Juni na kuibua mijadala ya kimataifa juu ya ubaguzi wa rangi.

Kulingana na Yasuko Takezawa, Profesa katika Chuo kikuu cha Kyoto, tatizo la ubaguzi wa rangi pia ni tatizo liliopo katika jamii za wajapan.

“Wajapani wengi hawana uzoefu wa moja kwa moja na watu weusi. Picha ya watu weusi nchini Japan inaonekana kupitia vyombo vya habari, vipindi vya tamthilia, sinema, na watu maarufu wa Afrika, au wachekeshaji wanaoigiza ubaguzi. Ni picha ambayo si sahihi”, alisema.

Mnamo mwezi Januari mwaka 2019, Mhandisi wa magari Stephen Estelle, mwenye umri wa miaka 25 aliondoka nchini Marekani kujaribu maisha nchini Japan.

Bila kuzungumza kijapan, aliishi mwaka mmoja mjini Tokyo, ambako alipata uzoefu wa wajapan na baadae alihamia kusini mwa nchi, kufanya kazi katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Okinawa.

Stephen alisema alikua na uzoefu mzuri na wajapan na kwamba mazungumzo na Wajapan mara nyingi huwa ni kutokana na udadisi walionao.

“Ninahisi kuwa watu wanataka zaidi kuzungumza na mimi ili wanidadisi. Wanauliza maswali, wanataka kujua kuhusu nywele zangu na utamaduni wangu. Ninadhani ni kitu kizuri, kwasababu wanajifunza na kwahiyo wanaweza kutatua ubaguzi,” alisema.

“Kuna watu ambao huvuka mipaka na kuingilia maisha yako binafsi, nilibaini kuwa tulikua na uzoefu unaofanana. Nilipozungumza na marafiki zangu weusi, niligundua kuwa tuna uzoefu unaofanana, tunapokwenda kwenye vyoo vya umma unakuta mtu usiyemjua anajaribu kukuchunguza, hii ni kutokua na heshima, kunakopita kiwango”, alisema.

“Sipaswi kuwa na hofu juu ya ghasia za polisi hapa, lakini Marekani kuna uungaji mkono zaidi, marafiki Wamarekani weusi, jamii, familia. Kama nikiondoka nyumbani peke yangu ninaweza kusimamishwa na polisi.

Jamaican Danielle Thomas, mwenye umri wa miaka 28, aliwasili nchini Japan mwaka 2016 na akaanza kufanya kazi kama mwalimu wa skuli ya chekechea katika mkoa wa Ibaraki, uliopo kilomita 82 kutoka Tokyo.

Akiwa anawashughulikia watoto wa kijapan, Danielle alisema ana uzoefu kufurahisha, kama vile mvulana aliyemwambia mama yake kwamba mwalimu wao ana uso wa rangi ya kahawia na mvulana mwingine aliyemuita mwalimu wa rangi ya kahawia.

Udadisi pia ni sehemu ya maisha yake ya kila siku nchini Japan. “Kila mara ninajibu maswali yale yale juu ya nchi yangu na hasa kuhusu nywele zangu, inanichosha, lakini sijali”, alisema.

Mbrazili Lorraine Eduarda Vital Cota Nakamura, mwenye umri wa miaka 28, alikwenda Japan akitokea São Paulo miaka miwili iliyopita baada ya kushinda hofu ya kuhamia sehemu nyingine ya dunia

“Wakati huo mume wangu anayezungumza kijapan hakuwa na kazi na wazo la kwenda Japan likaja. Niliogopa sana, niliamini kuwa wajapan ni wabaguzi na nilihofia sana maisha ya binti yangu ambaye alikuwa na umri wa miaka 6”, alisema.

Lorraina aliishi na familia yake katika mkoa wa Mie Prefecture, katikati mwa Japani. Mbrazili huyo alisema alianza kufanyakazi katika viwanda na alihisi kukaribishwa, lakini alikabiliwa na ugumu wa kuyazoea maisha, hasa kwasababu hakuifahamu lugha.

Lorraine alifungua saluni ya urembo, iliyojikita zaidi katika ususi wa nywele, rasta na nywele za kushonwa kichwani (weave). Anasema binti yake Helena ambaye sasa ana umri wa miaka 8 amezowea vyema maisha ya skuli nchini Japan, lakini alikabiliwa na kipindi cha unyanyasaji.

Kuhusu ubaguzi wa rangi, Lorraina alisema alipitia hali ngumu, hasa wakati alipokua akifanya kazi katika nguo za mitumba na kuwaomba baadhi ya watoto wajiangalie kwenye kioo

“Mama mmoja kati ya akinamama waliokuwepo alisema ‘abunai, abunai’ (ikimaanisha hatari kwa kijapani) na sikuelewa. Ni kama alikuwa anawaambia watoto kuwa mimi ni hatari kwao,” anakumbuka. Licha ya hayo anasema uzoefu wake kwa ujumla nchini Japan umekua ni mzuri.

Mnaigeria Samuel Lawrance, ambaye amekuwa nchini Japan kwa zaidi ya miaka 15 na amejichanganya binafsi katika jamii ya wajapani na mfumo wa nchi katika jamii ya wajapani, kwani ni kitu fulani ambacho hutokea kwa siri.

“Nimefanya kazi na kampuni ya kijapani miaka michache iliyopita na nikapitia hali ngumu sana, kumuona mtu ambaye hajafikia kiwango na uzoefu kuniliko akiwa bosi wangu kwasababu tu ni mjapani.

Hisia ni kwamba hata niwe na ujuzi bora wa aina gani, nifanye chochote kile siwezi kupanda cheo kwasababu mimi ni mgeni au kwasababu mimi ni mweusi”, alisema.