LONDON, England
KLABU ya Chelsea imemsaini beki wa kushoto wa England, Ben Chilwell akitokea Leicester kwa mkataba wa miaka miatno wa pauni milioni 45.

Chilwell anakuwa ingizo la tatu la msimu wa majira ya joto baada ya kuwasili kwa winga, Hakim Ziyech (27), kutoka Ajax na mshambuliaji Timo Werner (24), kutoka RB Leipzig.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 23, ni tunda la akademia ya Leicester ambalo lilianza mechi yake ya kwanza na klabu hiyo 2015, na alikuwa na mkataba na ‘Mbweha’ hadi 2024.

Alikosa mechi tano za mwisho za msimu wa 2019-20 kutokana na maumivu ya mguu.
Chelsea ilishika nafasi ya nne na kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na

kuiacha Leicester kwnye siku ya mwisho ya msimu wa Ligi Kuu ya England, mwezi Julai.
“Natarajia kuwa sehemu ya kikosi hichi kichanga, chenye nguvu kinachoongozwa na Frank Lampard huku tunapopigania heshima msimu ujao,” alisema, Chilwell ambaye ana michezo 11 akiwa na England.

Chilwell amecheza mechi 123 akiwa na Leicester na amefunga magoli manne, matatu miongoni mwa hayo yalikuja kwenye ligi msimu uliopita.(BBC Sports).