BEIJING,CHINA

MMILIKI  wa vyombo vya habari wa Hong Kong Jimmy Lai, amekamatwa jana kwa tuhuma za kukiuka sheria mpya ya usalama wa taifa.

Watoto wake wawili wa kiume na wakurugenzi kadhaa waandamizi wa kampuni inayochapisha magazeti yake, nao pia walikamatwa katikati mwa ukandamizaji wa hivi karibuni dhidi ya sheria hiyo.

Polisi ya Hong Kong ilithibitisha kupitia Twitter kwamba iliwakamata watu saba kwa tuhuma za kukiuka sheria hiyo mpya.

Polisi walisema kuwa makosa yanayoshukiwa ni pamoja na kushirikiana na nchi za kigeni na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea.

Sheria hiyo mpya ya usalama wa taifa iliyoanzishwa na China ilianza kutumika mwishoni mwa mwezi Juni, na inawalenga wale wanaotaka kujitenga, vitendo vya ugaidi, mapinduzi na kushirikiana na vikosi vya kigeni.

Adhabu ya makosa hayo ni kifungo cha miaka kumi jela.