Ataka wananchi wake wakoshe barakoa kwa petroli

DUNIA inaendelea kukabiliwa na janga la ugonjwa wa corona, ambapo kwa mujibu wa takwimu ugonjwa huo hadi Agosti 3 watu milioni 18,252,944 wameambukizwa maradhi hayo duniani kote.

Takwimu pia zinabainisha kuwa hadi tarehe hiyo kiasi cha watu 693,117 wamefariki ambapo watu wengine 11,455,858 wakiripotiwa kupona ugonjwa huo.

Janga la corona limetuwezesha kusikia kauli kutoka viongozi mbalimbali kwa mfano rais wa Marekani ambaye nchi ndiyo iliyoathiri zaidi na corona aliwataka wananchi wake watumie ‘chloroquine’ kama kinga na tiba ya corona.

Kwa bahati mbaya sana dawa hiyo aliyotaka rais watu watumie hata wataalamu hawajathibitisha kama kweli inaweza kutibu corona. Suali hili kwa kweli lilizua taharuki kubwa duniani hasa kusikia kauli hiyo ikitolewa na kiongozi mkubwa kabisa hapa duniani.

Hivi karibuni rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte ambaye ana utata na misimamo inayofanana na Trump ambaye nchi yake kwa wakati huu inapitia kwenye kipindi kibaya cha corona naye alitoa kauli ya kutatanisha sana.

Katika kukabiliana na ugonjwa wa corona nchini Ufilipino, Duterte ameaagiza wananchi wananchi wa nchi hiyo watumie petroli kuosha barakoa jambo ambalo ni kingwa dhidi ya maambukizi ya corona.

Rais huyo aitoa kauli hiyo wiki moja kabla ya kuirejea tena huku wakiwasisitiza wananchi wa taifa hilo kuhakikisha wanatekeleza amaria yake na kwamba hatanii na sio mzaha.

Duterte amelazimika kuirejea tena kauli hiyo baada ya hapo awali alipoitoa watalamu wa afya nchini Ufilipino waliielezea kama mzaha na kwamba wananchi wasichukulie kwa umakini.

Maofisa wa afya nchini humo waliwaeleza wananchi kwamba barakoa zilizotengenezwa kwa kitambaa cha nguo, zinatakiwa kuoshwa kama kawaida na zile barakoa nyengine zitumike mara moja tu na kutupwa.

Akionekana kuwa na msimamo na kupingana na wataalamu wa afya, Duterte rais huyo alisisitizia matamshi yake na kuongeza “kile nilichosema ni ukweli na sikuwa natania ama kuwafanyia mzaha, nendeni kwenye vituo vya petrol ziosheni barakao zenu”, alisema.