ADDIS ABABA,ETHIOPIA

ETHIOPIA imethibitisha kuwa idadi ya watu walioambukizwa COVID-19 nchini humo imefikia elfu 18.7,dinia inasisitizwa kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

Wizara ya afya ya Ethiopia ilisema kwenye taarifa yake kuwa watu zaidi ya elfu 7,607 walipimwa katika saa 24, 707 kati yao walikutwa na maambukizi.

Taarifa pia ilisema watu wengine 28 walikufa kutokana na ugonjwa huo na kufanya idadi ya watu waliokufa kwa ugonjwa huo kufikia 310, na waliopona walifikia 7,601 na wengine elfu,703 wanaendelea na matibabu.

Kampeni ya upimaji mkubwa ilianza, ambayo Serikali ya Ethiopia ilisema matokeo yake yatatumika kuamua hatua zinazofuata katika mwaka mpya unaoanza septemba 11.

Waziri Mkuu wa Ethiopia  Abiy Ahmed alisema kuongeza upimaji ndio njia pekee ya kujua mwelekeo wa maambukizi ya ugonjwa huo kitaifa, ili kuwezesha kufanya maamuzi yenye ufanisi kutoka pande mbalimbali.