BARCELONA, Hispania
MIAMBA ya soka ya Hispania, Barcelona, wamejipanga kutaka kumsajili beki wa Manchester City, Eric Garcia kwa ada ya euro milioni 27.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 19, amekua akipewa nafasi ya kucheza mara kwa mara na meneja wa Manchester City Pep Guardiola, na ameonyesha kuwa na uwezo mkubwa kisoka, lakini, mpaka sasa amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia matajiri hao wa mjini Manchester.

Uamuzi wa kugoma kusaini kandarasi mpya, umeifanya klabu ya FC Barcelona kuhitaji kumrejesha nyumbani kinda huyo, lakini, ada ya kumng’oa Etihad imekua kikwazo kwao.

Wakati klabu ya Manchester City wakitajwa kuwa wanahitaji euro milioni 27, kumuachia nyota huyu, Barcelona wamesema wapo tayari kulipa nusu ya gharama hiyo iliyotajwa.
Guardiola ameshathibitisha kuwa nyota huyo anataka kuondoka klabuni hapo, lakini, uongozi wa ManCity unahitaji kuepuka kumuachia aondoke kama mchezaji huru msimu ujao, hivyo watahitaji kutazama tena mpango wao.(BBC Sports).