NA TATU MAKAME

IKIWA leo maonyesho ya nanenane yanaanza katika eneo la Kizimbani Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja, Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini ‘B’ imesema itashiriki.

Msaidizi Mkurugenzi Kilimo,Maliasili, Mifugo na Mazingira Suleimain Khamis Suleiman, alisema hayo wakati alipozungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema halmashauri tayari imeandaa banda maalum litakalotumiwa na watendaji wa Ofisi hiyo kwa kutoa elimu kwa kutumia sinema kwa siku zote za maonyesho.

Alisema kuwa njia hiyo itarahisisha upatikanaji wa elimu kwa haraka hasa ukizingatia kuwa wakulima wengi bado wanaendelea kulima kilimo cha zamani na wanahitaji kupatiwa mbinu za kisasa za kilimo.

Ofisa mifugo halmashauri hiyo, Hassan Ibrahim Khamis, alisema watahakikisha wanatoa elimu ya ufugaji kwa wananchi wanaojihusisha na ufugaji katika wilaya hiyo, ili nao wanufaike na maonyesho hayo.