LISBON, Ureno
KLABU ya Inter Milan inayonolewa na Antonio Conte imefanikiwa kuingia fainali ya Ligi ya Europa, baada ya kuitandika Shakhtar Donetsk magoli 5-0.

Miamba hiyo iliongoza katika nusu ya kwanza kwa goli lililofungwa na Lautaro Martinez na katika kipindi cha pili, mvua ya magoli ikaendelea kunyesha baada ya Danilo D’ambrossio kuongeza goli jengine sawa na Martinez tena.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Romelu Lukaku akatingisha nyavu mara mbili. Lukaku ambaye alitimkia Italia kutoka Uingereza sasa ameifungia Inter magoli manane kwenye 10 za mwisho alizocheza kwenye mashindano mbalimbali.

Kwenye fainali hiyo, Inter sasa itakutana na Sevilla ya Hispania Cologne Ujerumani huku Manchester United na Shakhtar Donetsk wakikutana katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.(AFP).