TEHRAN,IRAN

WAZIRI  wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi hiyo inaweza kujikidhia asilimia 90 ya mahitaji yake ya kiulinzi kwa kiwango cha juu.

Brigedia Jenerali Amir Hatami aliyasema hayo mjini Tehran katika kikao na waandishi habari kwa mnasaba wa siku ya Sekta ya Viwanda vya Ulinzi na huku akiashiria sifa za kipekee za sekta hiyo.

“Sisi tunajikidhia zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji yote ya zana za kijeshi ambazo pia zinaundwa kwa viwango vya juu.” Alisema.

Alisema pamoja na kuwepo vikwazo vya kimataifa na changamoto za kifedha lakini wataalamu wa Irani waliunda zana za kiulinzi na hivyo nchi imejitosheleza katika sekta hiyo.

Alisema hivi sasa Iran inalenga kuwa nchi ya kwanza kwa mtazamo wa sayansi na teknolojia na kwamba wataalamu wako mbioni kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.

Brigedia Jenerali Amir Hatami alisema katika kipindi cha miezi michache ijayo Iran itarusha satalaiti katika anga za mbali kwa kutegemea makombora yaliyoundwa nchini.

Alisema kombora jipya la kubeba sataliti ambalo limeundwa Iran lina uwezo wa kubeba satalaiti iliyo na uzito wa zaidi ya kilo 100 na kuifikisha masafa ya juu katika anga za mbali zaidi ikilingnaishwa na sataliti zilizotangulia za Iran.