ZASPOTI
CHAMA cha Soka cha Ivory Coast, kimesema, kimeahirisha kabisa uchaguzi wa kuchagua rais mpya kwa sababu ya kile ilichokiita ‘mapungufu makubwa’ katika mchakato wa uchaguzi.
Uchaguzi, ambao ulipangwa kufanyika Septemba 5, umekumbwa na msururu wa matatizo.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, ni mmoja wa wagombeaji wa chama hicho, lakini, mwanzoni alikataliwa ruhusa ya kusimama kwa sababu ugombea wake hakuungwa mkono na chama cha wachezaji wa nchi za Afrika Magharibi. Drogba amepokea msaada aliohitaji kutoka kwa klabu kadhaa huko Ivory Coast.

Drogba mwenye umri wa miaka 42, nahodha wa zamani wa Ivory Coast na mfungaji anayeongoza kwa wakati wote, aliteka umati mkubwa wakati alipowasilisha maombi yake kwenye jengo la shirikisho mwanzoni mwa mwezi.

Wengine wawili wameomba kugombea uchaguzi huo, mjumbe wa kamati ya utendaji, Sory Diabate na makamu wa zamani wa shirikisho hilo, Idris Diallo. Tume ya uchaguzi ilitarajiwa kuthibitisha orodha ya mwisho ya wagombea wiki hii.
Chama hicho kitafanya mkutano mkuu mnamo Agosti 29.(Goal).