NA HADIJA WAZIRI

TIMU ya  Jamaika Mokaz imefanikiwa kuibuka kidedea  baada ya kuipa kichapo cha mabao 3-1 timu ya  Inter Milan.

 Mchezo huo  ni muendelezo wa ligi  ya Mafia Cup uliopigwa majira ya saa 10: 30  za jioni.

Pambano lililokuwa na ushindani, timu ya Jamaika Mokaz ilipata bao la mapema mnamo dakika ya tano lililowekwa wavuni na Inno Visenty.

Wakati bao la Pili lilifungwa na Hassan  Mkumbilo katika dakika ya 20, mabao ambayo yalidumu hadi hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili timu ziliendelewa kucheza kwa kushambuliana kila mmoja akitafuta bao,ambapo katika dakika ya 82 Yakub Hada aliongeza bao la tatu.

Bao pekee la kufutia machozi la  timu ya Inter Milan lilifungwa na Ali Nuhu kwenye dakika ya 87.

Mara baada ya kumaliza pambano  hilo Zanzibar leo ilifanikiwa kuzungumza na kocha wa Jamaika Mokaz Hamis Mohammed na kuwataka mashabiki kuonesha ushirikiano na wachezaji kwa ili kufanya vyema katika michezo mengine.