Lengo ni kubaini magonjwa na mapema
NA MWANDISHI WETU
IKIWA wanawake walio wengi wanaendelea kujitokeza katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja katika kupima matatizo yanayohusiana na na afya ya shingo ya kiazazi kama vile kuangalia dalili na ishara za saratani ya shingo kizazi na mambo mengine mengi yanayohusiana na magojnwa ya kike.
Lakini imekuwa tofauti kubwa sana na jamii ya kiume ambayo inahitaji kufanya upimaji yakinfu hasa kutokana na ugonjya mbaya wa saratani ya tenzi dume ambao unawakumba watu wengi duniani.
Inasemekana baada ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti basi saratani ya tenzi dume imechukuwa namba 3 duniani na kupoteza maelefu ya wanaume kutokana na vifo vingi vinavyosababishwa na saratani ya tenzi dume.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari nchini kilichonukuu Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kilisema kuwa asilimia 40 ya watu waliofanyiwa vipimo na Taasisi hiyo ya JKCI kwenye maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyofungwa hivi karibuni, kwamba asilimia 40 ya watu wamegundulika na shindikizo kubwa la damu, huku aslimia 20 wakiwa na sukari kwenye damu isio ya kawaida mwilini mwao na huku asilimia 60 ya watu hao wakiwa na uzito mkubwa.
Kwa mukhtaza huo basi makala haya ni namna gani inawatia motisha wanajamii kujua umuhimu wa kuchunguza afya zao na mapema.
Watu wengi huenda kupata huduma ya afya pale wanapokuwa hawajisikii vizuri au wana tatizo la kiafya linalowasumbua.
Kuna magonjwa makubwa ambayo hayaonyeshi dalili zozote hadi pale yanapokuwa yameshaenea au yameleta athari kubwa mwilini, hata kusababisha kifo ghafla, magonjwa haya ni pamoja na ugonjwa wa moyo, shinikizo kubwa la damu, kisukari, saratani nakadhalika.
Upimaji wa afya unaweza kupunguza athari zifuatazo katika mwili wa binaadamu ikiwa ni pamoja na maradhi yeyote hata kama yamejificha kiasi gani yanaweza kugundulika mapema na hivyo kuweza kutibika kwa urahisi zaidi.
Aidha unapogundulika mapema kama uko katika hatari ya kupata au una viashiria hatarishi (risk factors) vya magonjwa sugu.
Kwa mfano unaweza kugundulika kuwa una lehemu (cholesterol) nyingi mwilini au presha/ shinikizo la damu limepanda. Kwa maana hiyo basi viashiria hivi kama viatagundullika mapema vitadhibitiwa na hutoweza kupata magonjwa ya moyo.
Kupima afya yako wewe mwana jamii ni fursa pekee na nzuri yakuweza kujadiliana na muhudumu wa afya kama vile daktari au muuguzi juu ya matatizo madogo madogo ambayo yameonekana na hayana umuhimu wa kwenda hospitali lakini huathiri afya na maisha.
Aidha fursa hii huweza kuambatana kwa kupata ushauri ulio nzuri na manufaa tele katika kuboresha afya na maisha yako ya kila siku.
MAMBO MUHIMU YANAYOHITAJIKA KATIKA KUPIMA AFYA YAKO
Kuna mambo ambayo ni muhimu sana katika umri wowote ni mengine ni muhimu zaidi katika umri mkubwa.
Kupima afya mara nyingi kunategemea umri na jinsi ya mtu alivyo. Viafuatavyo ni baadhi tu ya vipimo muhimu katika kujuwa afya yako kama vile:-
KIPIMO CHA SUKARI MWILINI:(BLOOD SUGAR)
Kipimo na sukari kinatakiwa kufanyika kila baada ya miaka miwili hadi mitatu kwa mwaka na kila pale inapowezekena lakini kila umri uunapoongezeka kuanzia miaka 40 au zaidi inashauriwa kufanya vipimo mara kwa mara, sukari ya kwaida mwilini inatakiwa iwe 3.5 mpaka 6.9 mmol/l
SHINDIKIZO LA DAMU: (BLOOD PRESSURE)
Kipimo cha shindikizo la damu kinahitajika kufanyika kila mara unapokwenda hospitali. Hata hivyo, inashauriwa kufanyiwa kipimo hiki zaidi ya mara mbili kwa mwaka.
SHINGO YA KIZAZI: (CERVIX)
Wanawake kuanzia miaka 20 na kuendelea wanashauriwa kufanyiwa vipimo vya pap-smear au Visual Inspection of Acetic Acid (VIA) ili kuchunguzwa hali ya saratani kila baada ya miaka mitatu.
KIPIMO CHA SARATANI YA MATITI: (BREAST CANCER)
Wanawake wanashauriwa kwenda hospitali kufanyiwa uchunguzi wa matiti kwa njia ya x-ray (mammogram). Mara nyingi wataalam wa afya wanashauri mwanawake aliye na umri wa miaka kati ya 20-30 afanyiwe kipimo hiki kila baada ya miaka mitatu na yule mwenye umri wa miaka 40 na zaidi afanyiwe kipimo hiki kila mwaka.
Vile vile mwanamke yeyote mwenye umri kuanzia miaka 20 anatakiwa kujua na kujichunguza matiti yake mwenyewe kila mwezi
KIPIMO CHA TEZI DUME:(PROSTATE)
Kwa wanaume chini ya umri wa miaka 40 mara nyingi inashauriwa kufanyiwa kipimo kila baada ya miaka miwili au zaidi. Kwa wanaume walio na umri zaidi ya miaka 40 inashauriwa wafanye kipimo hiki kila mwaka.
LEHEMU (CHOLESTEROL)
Inashauriwa kipimo hiki kifanyike baada ya miaka miwili hadi mitatu kwa watu wenye umri wa miaka 40 au zaidi inashauriwa kufanya vipimo mara kwa mara. Kipimo cha kawaida cha lehemu ni kuanzia 3.1 mpaka5.2 mmol/l
KIPIMO CHA MOYO:
Ni vizuri mtu yeyote mwenye umri wa zaidi ya miaka 40 anashauriwa kufanya kipimo hiki mara kwa mara iwezekanavyo.
Vipimo vya moyo vinajulikana kwa jina kitaalmu ECG na ECHO na kupiga picha ya X -ray ya kifua kuangalia umbile la moyo.
KIPIMO CHA UZITO WA MWILI: (BODY MASS INDEX)
Kipimo cha uzito wa mwili hakina wakati muafaka hata hivyo unatakiwa ufuatilie uzito wako zaidi ya mara mbili kwa mwaka.
Kipimo hichi hupimwa kutokana na uwiyano wa uzito na urefu kwa fmuonekano maalumu ambao ni sawa na uzito katika kilo gawanya na urefu katika mita square, Mfano mtu mwenye kilo 60 na urefu wa sentimita 158
Aidha BMI = 60/1.58 ambazo ni sentimita square =60/2.5 = 24 kwa bodi masinde hii mtu huyu atakuwa na uzito wa kawaida.(Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani.
KIPIMO CHA KIZAZI
Ni muhimu sana kufanya vipimo vya uzazi hasa kwa wale wenza ambao wameowana kujuwa vipi katika hali ya uzazi wao uko imara au la hii itaondosha zana potofu na malumbano baina ya wapenzi hawa wawili pindipo itatokozea changamoto katika kutafuta kizazi, na itakuwa rahisi kupata tiba mapema kama itakokezea mmoja wao ataonekana na tatizo.
MAMBO YA KUZINGATIA MBALI NA UPIMAJI WA AFYA YAKO
Ikumbukwe kwamba mbali na utaratibu mzuri na wa hiyari wa kupima afya yako bado jamii na wasomaji wa makala hii wanatakiwa kuzifuata kanuni zote za afya ili kupiga vita adui maradhi kama vile ufanyaji wa mazoezi ya viungo, kulala mapema na kujihifadhi na chandarua pale inapobidi na kupumzika.
Badili mtindo wa maisha, kula chakula ambacho haikijakobolewa, usivute sigara, usitumie vinywaji vyenye vilevi, kuwa na utamaduni wa kusafisha mazingira tunayoishi, usafi wa mwili, tumia maji safi na salama, nawa mikono kabla na baada ya kula, tumia vyoo kwa uangalifu zaidi, usitupe taka taka ovyo zihifadhi sehemu husika na baadae zipige moto au kuzifukia.
Na kwa upande wa watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano, wazee na walezi wanatakiwa kudumisha mahudhurio yao ya kawaida ya kliniki kwa kupata chanjo pamoja na kujua/kusimamia maendeleo na ukuaji wa mtoto.
INDHARI
Utaratibu wa kupima afya zetu mara kwa mara, itasaidia kupunguza magonjwa hasa yale yasiyoambukiza, inashauriwa kupima afya angalau mara moja kwa mwaka.
Hata hivyo, kama mtu ana viashiria hatarishi vya kupata magonjwa sugu mtaalam wa afya atamshauri ni mara ngapi apime afya yake.