HIROSHIMA, JAPAN

JAPANI imeadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 75 ya bomu la atomiki la Hiroshima, huku meya wake akihimiza ulimwengu kuungana dhidi ya vitisho kwa ubinadamu ikiwa ni pamoja na ile ya silaha za nyuklia.

Meya wa Hiroshima Kazumi Matsui alisema nchi zinapaswa “kuweka kando tofauti zao na kukusanyika pamoja ili kushinda changamoto za wanadamu na za asili.”

“Asasi za kiraia lazima kuungana dhidi ya vitisho vyote,” Matsui alisema katika sherehe ya kila mwaka katika Ukumbusho wa Amani.

Maadhimisho hayo yamefanyika kimyakimya kutokana na maambukizo ya COVID-19 huko Japan.

Hata hivyo, ukimya wa muda ulizingatiwa na wale walihudhuria, pamoja na Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe, ambae alihudhuria majira ya saa 8:15 asubuhi wakati ambapo bomu la “Little Boy” liliripuka huko Hiroshima mnamo Agosti 6. , 1945.

Bomu hilo liliwauwa watu takriban 140,000 hadi kukamilika mwaka huo wa 1945.

Licha ya Japan kutokuwa na saini kwa Mkataba wa Kuzuia Silaha za Nyuklia, Abe, katika hotuba yake, alisema nchi hazipaswi kuacha msimamo tofauti wa mataifa juu ya silaha za nyuklia kuongezeka zaidi.

“Kila nchi lazima ipongeze juhudi za kuondoa hali ya kutoaminiana kwa kuhusika kwa pande mbili na mazungumzo kati ya mazingira magumu ya usalama na kuongezeka kwa tofauti kati ya nafasi za mataifa juu ya silaha za nyuklia,” Waziri Mkuu wa Japan alisema.

Idadi ya walionusurika katika milipuko hiyo ya mabomu ya atomiki ikiwa ni pamoja na Nagasaki inayojulikana kama ‘Hibakusha’ni wastani wa miaka 75 sasa machungu yake kwa wanusurika yanaonekana hadi sasa.