LONDON,UINGEREZA

WAZIRI Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametahadharisha kuhusu athari mbaya za kujitenga Scotland na Uingreza.

Alisema kuwa iwapo muungano wa mataifa manne yanayounda Uingereza yaani England, Scotland, Wales na Ireland ya Kaskazini, utavunjika nchi hiyo itakuwa dhaifu zaidi.

Katika kura ya maoni ya kujitenga Scotland na Uingereza iliyofanyika mwaka 2014, asilimia 55 ya wananchi wa eneo hilo walipinga suala hilo na asilimia 45 waliafiki kujitenga na Uingereza.

Hata hivyo kujiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya tarehe 31 Januari mwaka 2020 na kuwepo ufa na tofauti kubwa za kukabiliana na corona katika maeneo mbalimbali ya Uingereza vilizidisha hisia za kujitenga kwa baadhi ya mataifa ya Uingereza.