NAIROBI,KENYA

KENYA ameishukuru China kwa msaada wake kwenye kuimarisha juhudi dhidi ya COVID-19.

Katibu mkuu wa Wizara ya afya ya Kenya Rashid Aman, alisema Serikali ya China na mashirika mbalimbali walitoa misaada ya vifaa vya matibabu kwa Kenya ili kuongeza uwezo wake wa kupambana na COVID-19.

Aman alisema moja ya michango muhimu ni vifaa vya upimaji vilivyotolewa na Jack Ma, ambavyo vimekuwa msingi wa mpango wa upimaji wa nchi hiyo.

Aman alisema Kenya inaweza kuiga uzoefu kutoka China, ambayo ilichukua hatua nyingi za kuzuia kuenea kwa COVID-19.