NAIROBI, KENYA

SHIRIKA la ndege Kenya limepanga kurejesha tena huduma zake za usafiri wa ndege kwa safari za kimataifa kutoka ndani ya nchi hadi New York kuanzia Oktoba mwaka huu.

Mwenyekiti wa Shirika hilo Michael Joseph alisema,huduma za usafiri wa ndege za Kimataifa zitaanza kulingana na mahitaji  ya watu wanaotaka kusafiri.

“Nahisi tutakwenda mara moja kwa wiki na kama kutakuwa kuna mahitaji makubwa,tutakwenda mara mbili au tatu kwa wiki.Lakini sijui ni lini tutarudisha safari za kila siku Marekani kutokana na janga la corona”,alisema Joseph.

Ukosefu wa ndege za moja kwa moja unawafanya abiria kutoka Kenya kwenda Marekani kubadilisha ndege Uingereza safari ambayo inaweza kuchukua hadi masaa 20.

Mamlaka ya Viwanja vya ndege vya Kenya ilipokea ndege ya Lufthansa, British Airways na ndege za KLM  kwa mara ya kwanza tokea kufunguliwa kwa ndege ya Kenya ya Kimataifa.

Akizungumza katika hafla ya mapokezi ya ndege hizo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja hivyo Alex Gitari alisema,mamlaka hiyo imepoteza asilimia 80 ya biashara zake zinazotokana na abiria wa kimataifa.

Alisema kupungua kwa mapato ya  kiwango cha kimataifa inakadiriwa kuwa ni Zaidi ya dola bilioni 97 ,kwa mwaka 2020.

Nchi inasimamia taratibu za usafiri wa ndege ili kusaidia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona pamoja na kuhakikisha kwamba sekta hiyo inafunguliwa kwa kufuata masharti yaliyowekwa na Wizara ya afya.

Gitari alisema  abiria wanaowasili Kenya watalazimika kuwa na vyeti vya kuthibitisha kwamba hawana Covid-19 kabla ya masaa 96 ya kuondoka kwa ndege .

Abiria wanaotoka Kenya wanapaswa kufata sheria na taratibu zilizowekwa katika nchi wanazokwenda pindi wakiruhusu safari za kimataifa.