NAIROBI,KENYA

RAIS  Uhuru Kenyatta wa Kenya amezindua jukwaa la Umoja wa mataifa ambalo  litaisaidia Serikali kufungua fursa kwa ajili ya vijana wa Kenya.

Rais Kenyatta alisema vijana wanachukua robo tatu ya idadi ya wakenya wote, na kuongeza kuwa kwa miaka kadhaa sasa Serikali imeongeza uwekezaji kwenye sekta zinazotegemea vijana kama vile elimu, Tehama na ujasiriamali, ikiwa ni njia ya kutambua nguvu kubwa yenye uwezo wa kuchochea uchumi walionao vijana.

Jukwaa la Generation Unlimited ni mpango wa Umoja wa mataifa wa kuwawezesha vijana ulioanzishwa mwaka 2018, ukiwa na lengo la kuwahakikishia vijana wenye miaka kati ya kumi na 24, wako skuli au wawe wameajiriwa kabla ya mwaka 2030.

Rais Kenyatta alisema jukumu kubwa la Serikali yake ni kuleta ajira na maisha endelevu kwa vijana.