NA KHAMISUU ABDALLAH

HAKIMU Mdhamini wa Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Mohammed Subeit ameiahirisha kesi inayowakabili ndugu wa familia moja waliodaiwa kuvunja ukuta, hadi Septemba 9 mwaka huu.

Mahakama iliiahirisha kesi hiyo kutokana na ombi lilotolewa na upande wa mashitaka kuiomba mahakama kuhairishwa kwa ajili ya kuwasilisha mashahidi.

Washitakiwa hao ni Abdalla Ali Hassan (45) na Khamis Ali Hassan (37) wote wakiwa wakaazi wa Chukwani wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Ilidaiwa kuwa huko Chukwani washitakiwa hao wote kwa pamoja bila ya halali na makusudi walivunja ukuta wa nyumba unaomilikiwa na mlalamikaji Said Gharib Bilal kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Ndugu hao walidaiwa kuwa makusudi, wamedaiwa kuvunja ukuta huo wa Said Gharib Bilal huko katika maeneo ya Chukwani wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja majira ya saa 3:00 asubuhi.

Mwendesha Mashitaka Wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Mohammed Haji Kombo ambae alidai kuwa tukio hilo walilitenda January 3 mwaka jana.

Kosa la kuharibu mali kwa makusudi ni kinyume na kifungu cha 326 (1) cha sheria namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar.

Shitaka hilo walisomewa na

Washitakiwa hao wapo nje baada ya kutimiza masharti waliyopewa mahakamani hapo kwa kujidhamini wenyewe kila mmoja kwa shilingi 1,000,000 za maandishi na wadhamini wawili ambao kila mmoja waliwadhamini kwa kima hicho hicho cha fedha za maandishi pamoja na kuwasilisha vitambulisho vyao vya Mzanzibari Mkaazi na Barua za Sheha wa Shehia wanazoishi.