NA MWAJUMA JUMA
TIMU ya soka ya Kilimani City imenusurika kushuka daraja baada ya juzi kushinda mabao 2-1 dhidi ya timu ya Mchangani.
Timu hiyo ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza Kanda ya Unguja ilishuka dimba la Mao Zedong na kuondoka na ushindi huo.
Kilimani City ililazimika kushinda kwenye mchezo huo ili kujinusuru kushuka daraja hilo ushindi ambao umewafikisha pointi 29.
Kufuatia matokeo hayo City imesalimika na badala yake Bweleo imechukuwa nafasi hiyo ya kushuka daraja.
Jumla ya timu nne zimeshuka daraja katika ligi hiyo ambazo sasa zitarudi katika mikoa yao kushiriki ligi daraja la pili Mkoa.
Timu hizo zilizoshuka ni pamoja na Kikwajuni, Miembeni, Bweleo na Mundu ambazo zinatoka katika mikoa tofauti.