PYONGYANG, KOREA KASKAZINI

KIM Jong Un, ambae ni kiongozi wa juu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK), amemteua Kim Tok Hun, kama Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, Shirika rasmi la Habari la Korea Kusini liliripoti Ijumaa.

Kim Tok Hun,

Kim Tok Hun aliteuliwa kuchukua nafasi ya Kim Jae Ryong baada ya kutangazwa kwa amri hiyo katika mkutano wa siasa wa Chama cha Wafanyakazi wa chama tawala, ambao uliongozwa na Kim Jong Un, ripoti hiyo ilisema.

Kim Tok Hun alikuwa mkuu wa kamati ya bajeti ya bunge kabla ya uteuzi mpya, ripoti hiyo haikuelezea sababu ya uingizwaji huo.