NA ASIA MWALIM

MAHAKAMA ya mwanzo Mwanakwerekwe, imempandisha katika kizimba cha mahakama hiyo Abdallah Shaib Khamis (32) mkaazi wa Amani Unguja, kwa kosa la kuweka gari sehemu hatarishi.

Abdallah alipandishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Suleiman Jecha Zaidi na kusomewa shitaka hilo na Mwendesha Mashitaka Koplo wa Polisi Mwalim Gharib.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, kufanya hivyo ni kinyume na kifungu cha 143 cha sheria namba 7 ya mwaka 2003 sheria za Zanzibar.

Mahakama ilidai kuwa, mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 2 mwaka huu, majira ya saa 11:00 jioni maeneo ya Michenzani, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Ilidaiwa kuwa, siku hiyo aliendesha Gari ya abiria inayokwenda njia namba 510 yenye namba za usajili Z.706 DL, akitokea upande wa Kisonge kuelekea upande wa Mkunazini, ikiwa amesimamisha gari hiyo kati kati ya barabara na kapakia abiria