NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya soka ya Raskazone imeshindwa kutamba mbele ya timu ya Kombaini ya Wilaya ya Mjini kwa kufungwa mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa  Mao Zedong juzi.

Mchezo huo ambao ni maandalizi kwa timu hiyo ya vijana inayojiandaa na mashindano ya vijana ya Rolling Stone yatakayofanyika Morogoro.

Katika mchezo huo Kombaini hiyo ambayo ipo chini ya mwalimu Mohammed Seif Kingi na wasaidizi wake wawili Ali Bakari Mngazija na Khamis

Gulity na kocha wa makipa Saleh Ahmed Machupa hadi inakwenda mapumziko ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili kilipoanza timu hiyo ambayo mbali na kujiandaa na mashindano hayo, lakini pia inajiandaa na mchezo maalumu ulioandaliwa na Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF utakaochezwa Agosti 8, mwaka huu dhidi ya Mlandege.