Viongozi wa dini wahimiza wananchi kudumisha amani uchaguzi mkuu

Na Maria Inviolata
MNAMO mwishoni mwa Oktoba mwaka huu wazanzibar na watanzania kwa ujumla wanatarajiwa kuwachagua viongozi watakaoiongoza nchi kwa miaka mitano ijayo.

Ili kuona kwamba uchaguzi unakuwa wa amani na utulivu daima viongozi wa dini kwa nafasi yao wamekuwa wakihimiza utulivu na mshikamano walionao watanzania hasa katika kuelekea uchaguzi na baadala ya uchaguzi huo.

Hivyoewe mpiga kura mtarajiwa ukifanya uchaguzi ufaao unachopata nini hasa? Una uhakika gani na uchaguzi huo?  NI furaha!  ukiwa na kusudi halisi la kuishi, kujua unakoelekea! Ni amani ya akili na moyoni inayoletwa na uhakika wa kwamba hakuna mwendo mwingine ulio bora zaidi ambao ungeweza kufuata.

Uchaguzi nini?  Ni mchakato wa kumchagua mtu kwa nafasi maalumu katika jamii  kicheo na kimajukumu yanayotokana na cheo hicho.

Uchaguzi hufanyika kwa nafasi za uongozi au nafasi za mamlaka Fulani ambapo mara nyingi  hufayika kwa njia ya kupiga kura kwa wenye haki ya kupiga kura.

Katika chama, jumuiya binafsi au klabu ni wanachama wanaowapigia kura kamati ya uongozi, mwenyekiti na maafisa wengine ambapo katika shirika za hisa ni wenye hisa wanaopigia kura uongozi.

Mpiga kura iheshimu kura yako! Kwa mfano kura ya Seneta Edmund G. Ross kutoka Kansas ilimuokoa Rais wa 17 Marekani Andrew Johnson katika mashtaka  yaliyokuwa yanamkabili tarehe 26, Mei mwaka 1868, nguli huyo Mhariri na Mchapishaji hakujali nini kitakachosemwa na kumtokea baada ya msimamo wake huo ulioshangaza wengi na kuibua mijadala duniani.

Nchi yenye demokrasia ya kweli huzingatia masuala ya uchaguzi, huhimiza na kuruhusu haki za kiraia na kisiasa kama vile uhuru wa kuongea, uhuru wa habari na kupata habari hizo, uhuru wa  kukusanyika, kutoa maoni, kuabudu, kushiriki na kusisitiza utawala wa sheria, utawala wa walio wengi pamoja na kuheshimu haki za wachache,  kutii mamlaka na kuikosoa kwa njia salama na haki.

Uchaguzi wa viongozi wa Serikali ni hitaji la kikatiba na takwa la demokrasia. Kama inavyoeleweka demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya umma.

Katika dola ni raia au wawakilishi wao wanaochaguliwa kutegemea nan chi husika kwa mujibu wa katiba na sheria zao za nchi.

Kwa mfano hapa Tanzania Uchaguzi wa viongozi wakuu ni (Rais) Makamu mtarajiwa na viongozi wengine.

Aidha uchaguzi kama huu huwahusisha wabunge,wawakilishi na madiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Siasa ya vyama vingi na demokrasia nchini zilianza mwaka 1992 baada ya kupitishwa kwa Sheria ya Vyama vya Siasa mwaka 1992.

Baada ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa uchaguzi wote ukiwamo wa Serikali za Mitaa zilihusisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

Wakati mwingine wananchi hushiriki moja kwa moja, hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwa mujibu wa sheria. Wakati mwingine huwakilishwa na viongozi wao waliowachagua.

DINI INAZUNGUMZIAJE UCHAGUZI?
Uislam unakubaliana na suala  la upigaji kura na unawahimiza Waislam kupiga kura.

Kwa mujibu wa Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Salum, anasema upigaji kura unakumbusha Waislam pale ilipopigwa kura ya Wakfu wa malezi ya Maryam bint ‘Imraan, ikabidi wafanye kura ya kutupa kalamu zao walizokuwa wakiandikia Taurati katika mto wa Jordan.

Yule ambaye kalamu yake itaelea katika mto ndiye atakayemlea Maryam. 

Walipozitupa kalamu zao, zote zilizama isipokuwa ya Nabii Zakariyyah ambaye pia naye alikuwa  ni Mtume wao.

Sheikh Ahad pia anasema kupiga kura kwa Waislam kunawakumbusha jinsi Mtume Muhammad (SAW) alivyokuwa akipiga kura ni mke gani wa kutoka naye.

Aidha Sheikh Ahad anasema kura kwa Waislam pia inarejea kisa cha Nabii Yunus aliyemezwa na samaki aina ya chewa  alipowakimbia watu wake, Yunus (amani iwe juu yake) alighadhibika na kuamua kupanda jahazi baharini, lakini jahazi hilo likakumbwa na mtikisiko wa bahari na kuyumba kwa kuzidiwa uzito hadi wasafiri waliomo ndani yake kukaribia kughariki.

Kutokana na hali hiyo, wasafiri wakashauri ipigwe kura, na ambaye kura itamwangukia basi ndiye mwenye nuksi na watamtumbukiza baharini ili wapate wepesi katika safari yao.

Kwa mara ya kwanza walipopiga kura ilimwangukia Nabii wa Allah Yunus (amani iwe juu yake). Mara ya pili ikamwangukia tena Yunus. Hivyo, akataka kuvua nguo zake na kujitupa baharini mwenyewe lakini wasafiri wenzake wakamkatalia kufanya hivyo Kisha wakarudia tena kupiga kura mara ya tatu, na kwa mara nyingine kura ikamwangukia Yunus.

Na hii iliyokea kwa sababu kuna jambo kubwa Allah alitaka litokee kwa Nabii Yunus. Allah aliyetukuka anasema: “Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume. Alipokimbia katika jahazi lililosheheni. Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walioshindwa.

Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa” (Qur’an, 37: 139- 142). Yunus alitumbukizwa katika bahari, na Allah aliyetukuka akamwamuru samaki mkubwa sana wa bahari ya kijani ammeze Nabii Yunus.

Vilevile, Allah aliyetukuka alimwamuru samaki huyo asimtafune na wala asivunje mifupa yake. ”Huyu Yunus si riziki yako.” Hivyo, akammeza na kuzunguka naye bahari zote.

“Wakasema: Yunus alipothibiti katika tumbo la samaki alidhani ya kuwa amekufa, akatikisa viungo vyake vikatikisika, ghafla akajikuta yu hai.

Hivyo akamnyenyekea Mola wake kwa kusujudu na kusema: ‘Ewe Mola wangu, ewe Mola wangu nimekujaalia msikiti katika sehemu ambayo hajawahi kukuabudu wewe yeyote”(Taz: Kisasaul Anbiyaai uk 329).

Ghafla, Nabii Yunus (amani iwe juu yake) akastushwa kwa kujikuta yupo katika viza vitatu, kiza cha usiku, kiza cha kina cha bahari na kiza cha ndani ya tumbo la samaki.


Hapa Yunus akahisi kosa lake na kukubali yakuwa amefanya kosa, pale alipotoka katika mji wa Ninawaa bila ya idhini ya Allah aliyetukuka.

Hivyo, ikawa anaswali na kuleta tasbihi na kumtaka msamaha Allah aliyetukuka akiwa katika tumbo la samaki. Uwezekano wa Yunus kubaki katika tumbo la samaki hadi Siku ya Kiyama ulikuwepo, lakini kulikuwa na jambo moja tu lilimuokoa kutoka katika adhabu hii chungu, nalo ni kumsabihi, na kumdhukuru Allah pamoja na kuleta dua. Allah anasema:

“Na ingeli kuwa hakuwa katika wan a o m t a k a s a Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka angelikaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa“ (Qur’an, 37: 143-144).


Hivyo, Sheikh Alhad anatoa wito kwa Waislam nchini kumuomba Mwenyezi Mungu awajalie Viongozi bora, kwa sababu kutegemeana na matendo yao wanaweza kujaliwa Kiongozi mbaya au mwema.

Anafafanua hivi: Iwapo Waislam  watafuata matendo mabaya basi wanaweza kujaliwa kiongozi mbaya ili awatese kutokana na matendo hayo, lakini wakapokuwa na matendo mazuri basi watajaliwa Kiongozi mwema.

DINI YA KIKRISTO NAYO INASEMA KATIKA MAANDIKO YAKE KUWA
Kupiga kura katika uchaguzi wa kisiasa, wafuasi wa Kristo yaani “Wakristo” wanaheshimu haki ya watu wengine ya kupiga kura, wao hawashiriki maandamano ili kupinga uchaguzi bali huishauri na kushirikiana na wenye mamlaka waliochaguliwa au kushauri mamlaka husika kufanya uchaguzi wa haki wao wanatambua fika kwamba hakuna Serikali timilifu duniani, ndiyo maana hawaungi mkono upande wowote katika shughuli za kisiasa za mataifa yao. (Mathayo 22:21; 1 Petro 3:16).

Je! Mkristo anapaswa kufanya nini katika nchi ambako kupiga kura ni lazima au kunapokuwa na uhasama kwa wale ambao hawaendi kwenye vituo vya kupiga kura?.

Mkristo huyo anaweza kukata kauli  kwa sababu Shadraki, Meshaki, na Abednego walienda hadi kwenye nchi tambarare ya Dura, basi anaweza kwenda kwenye kituo cha kupiga kura dhamira yake ikimruhusu.

Hata hivyo, atahakikisha kwamba halegezi msimamo wake wa kutounga mkono upande wowote wa kisiasa kwa kuchagua kiongozi bora.

Naye Yesu Kristo mtu mwenye mvuto na ushawashi zaidi katika historia ya dini ,hebu  fikiria kama ungemuuliza swali hili, Je, dini inapaswa kujihusisha na siasa? Yesu angejibuje? Akiwa duniani alijibu swali hilo kupitia maneno na matendo yake, kwa mfano katika mahubiri yake maarufu ya Mlimani Yesu alitoa miongozo inayoweza kuwasaidia wafuasi wake kutambua jukumu wanalopaswa kutimiza katika jamii tuchunguze mahubiri hayo.

Waandishi wa vitabu vya Injili wanataja matukio  kadhaa katika  huduma ya Yesu iliyokabiliane moja kwa moja na siasa, kwa mfano muda mfupi baada ya Yesu kubatizwa akiwa kijana wa miaka 30 Ibilisi alitaka kumpa cheo cha mtawala wa ulimwengu, katika huduma yake umati ulitaka kumgeuza Mfalme.

Baadaye watu walijaribu kumlazimisha kuwa mwanasiasa, Yesu alitendaje? Vitabu hivyo vinataja Ibilisi alitaka kumpa Yesu utawala wa “Falme zote za ulimwengu “, fikiria mambo ambayo Yesu angefanya ili kuwaondolea wanadamu mateso ikiwa angetumia mamlaka ya mtawala wa ulimwengu!

Bila shaka mtu yeyote anayeamini siasa ndiyo inayoweza  kusuluhisha na kutatua matatizo ya wanadamu na  anatamani kuyaondoa kamwe hangekataa cheo  kama hicho. Lakini Yesu alikataa – Matayo 4:8-11.

Watu walioishi wakati wa Yesu walitamani  sana kuwa na mtawala ambaye angeweza  kutatua matatizo yao ya kiuchumi  na kisiasa, kwa sababu walivutiwa na uwezo wa Yesu, walitaka mwanaume huyo ajihusishe na siasa.

Yesu alitendaje?  Mmoja wa waadishi wa Injili Yohana anasema “Yesu akijua wanataka kumkamata na kumgeuza mfalme  akaondoka tena kwenda milimani akiwa peke yake”.

(Yohana 6:10-15) ni wazi Yesu alikataa kujihusisha na siasa bali alitoa miongozo inayoweza kuwasaidia wafuasi wake na Wakristo kutambua jukumu wanalopaswa kutimiza katika jamii iliyowazunguka. Alisema hivi.

“Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikipoteza nguvu zake,ladha yake itarudishwaje? Haitumiki tena kwa kitu chochote bali ni ya kutupwa nje ili ikanyagwe kanyagwe na watu.  Ninyi ndio nuru ya ulimwengu …… Acheni  nuru yenu iangaze mbele ya watu ili wapate kuona matendo yenu  na kumpa utukufu Baba yenu  aliye mbinguni.”(Matayo 5:13-16).

Kwa nini Yesu alisema wafuasi wake ni kama chumvi na nuru? Maneno ya Yesu ni kama chumvi kwa wanadamu wote, bali si kwa kikundi fulani. Wao ni kama nuru, si kwa watu wachache, bali ka watu wote. Kwa kutumia maneno hayo ya mfano, Yesu alionyesha waziwazi kwamba hakutaka wafuasi wake wajitenge na jamii. Kwa nini? fikiria mambo yafuatayo Chumvi haiwezi kuhifadhi chakula ikiwa hatachanganywa na chakula chenyewe.

Aidha taa haiwezi kuangaza chumbani kama haitawekwa ndani ya chumba hicho, ni rahisi kuelewa kwa nini yesu hakuwaamuru wanafunzi wake wajitenge na kwenda katika sehemu fulani tu ya dunia ili kuanzisha jamii za waamini.

Kamwe hakuwaambia wafuasi wake wajitenge na watu ulmwenguni na waishi katika mashirika ya kidini.

Badala yake, kama vile chumvi inavyopaswa kugusa chakula na pia nuru inavyopaswa kuangaza gizani, ndivyo wafuasi au Wakristo wanavyopaswa kuwasaidia watu wenginena kuboresha maisha yao.

Wafuasi wa Kristo wa kweli zama hizi hawashiriki  siasa kwa sababu wanaiga mfano wa Yesu, alisema  hivi: “ Mimi si sehemu ya Ulimwengu”, akaendelea kuasa wafuasi wake hivi: “ Ninyi si sehemu ya Ulimwengu”. (Yohana 15:19;17:14).

Aliagiza wafuasi wake kushirikiana na watu wengine Wakristo wa kweli wanajitahidi sana kufuata kanuni  na sheria zaI nchi, Waroma 13:1-7. Unaposoma mistari hiyo unatambua kwamba “mamlaka zilizo kubwa” zinazotajwa ni Serikali za ulimwengu.

Maadamu Yehova anaruhusu serikali hizo za ulimwengu ziendelee kuwapo kwa sababu zinatimiza mambo muhimu kwa mwanadamu kama vile utaratibu fulani na kutoa huduma muhimu za jamii, mistari hiyo inawahimiza Wakristo wa kweli kuheshimu na kutii mamlaka hizo kama vile kutii sheria, kulipa kodi zote zinazohitajika, kujaza kwa usahihi fomu au karatasi zozote zinazohitajiwa na serikali, kutii sheria zozote zinazohusu familia, biashara, au mali za Serikali na binafsi.

Aidha kuheshimu mamlaka za ulimwengu kupitia mwenendo wa raia. Nyakati zingine huenda ukashughulika moja kwa moja na maofisa wa serikali. Mtume Paulo alishughulika na watawala kama vile Mfalme Herode Agripa na Gavana Festo. Watu hao walikuwa na udhaifu mkubwa, lakini Paulo alizungumza nao kwa heshima. (Matendo 26:2, 25.

Kwa mantiki hiyo basi waumini wa dini zote hawana budi kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa salama na amani hasa kwa wale wenye haki ya kuchagua.