WAPENZI wasomaji wetu wa Zanzibar Leo, katika safu yetu hii ya tiba asilia leo hii nimewatayarishia umuhimu wa kunywa maji ya uvuguvugu nyakati za asubuhi.

Kama hujaanza jaribu leo nawe utaona faida yake, basi fuatana katika faida sita za kunywa maji hayo.

Inawezekana unatumia kikombe cha chai au kikombe cha kahawa kila siku asubuhi, wengi wao hutumia maji ya kawaida ili kuanza siku vizuri.

Hivi vitu vimekuwa ndio tabia ya kila siku , hata hivyo wachunguzi wanasema kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi wakati tumbo halina kitu unapata faida za kiafya zaidi.

Madaktari wanashauri kutumia maji ya uvuguvugu yaliotiwa liau au ndimu ili kupunguza kalshiyamu ndani ya mwili. Kutumia maji ya moto inaongeza na kufungua utumbo ili kukufanya wewe upate haja kubwa kwa urahisi

Na hapa kuna faida 7 za vitu vinavyotokea katika mwili wako utakapoanza kutumia maji ya moto kila asubuhi.

1. YANASAIDIA KUONDOA MIKUNJO.
Kunywa maji inakusaidia usizeeke mapema,hakuna mtu anaependa kuzeeka mapema.hata hivyo sumu ndani ya mwili inaweza kukufanya uzeeke mapema.

Wakati mwili wako unapotoa sumu utapunguza magonjwa na uzee. Maji ya moto husaidia kuondoa sumu na yanasafisha kabisa. Zaidi sana yanasaidia kurejesha cells za ngozi iwe inaonekana kuvutia na nyororo.

2. HUEPUSHA MAUMIVU.

Dawa ya nguvu ya kutegemea kupunguza maumivu wakati wa hedhi ni maji ya moto, yanafanya misuli ya tumbo irilaksi na kupungua kwa maumivu. Maji ya moto husaidia mzunguko kapirali na misuli katika mwili pia.

3. YANASAIDIA KUPUNGUZA UZITO.


Inawezekana unajaribu kupunguza uzito na umesikia kuwa maji ya moto asubuhi yanaweza kuwa ni msaada mkubwa kwako. Hii ni kweli., maji ya moto yanaongeza joto la mwili, ambalo linabadilisha ongezeko la kiasi cha metabolic, kuongezeka kwa metabolic mwili unakuwa na uwezo wa kuchoma carories siku nzima.

Kama ukianza na kunywa maji ya moto yenye limau. Utausaidia mwili wako kuvunja vunja mafuta yalioko ndani.

4. YANABORESHA USAGAJI WA CHAKULA.

Unapokunywa maji ya moto asubuhi unasaidia kusisimua misuli na usagaji wa chakula na kujiskia uko imara zaidi.

Wacha kabisa kunywa maji ya baridi baada ya kula chakula, kwani kuna uwezekano mkubwa wa kusimamisha usagaji wa chakula chako kwa haraka, mwili wako ukawa na matatizo, maana maji ya baridi yanagandisha mafuta yalioko kwenye chakula na kufanya usagaji iwe ngumu kwako. Ni bora ukatumia maji ya moto kuliko ya baridi.

5. YANABORESHA MZUNGUKO WA DAMU MWILINI.

Kunakuwa na mlimbikizo wa mlolongo wa nervous na mlimbikizo wa mafuta mwilini, lakini unapotumia maji ya moto yanaenda kuondoa hio migandanizo. Hii hatua inatoa sumu yote ndani ya mwili na kuufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri na kufanya misuli kupumzika.

6. YANAKUFANYA UPATE USINGIZI VIZURI.

Unapotumia maji ya moto wakati wa chakula cha usiku, na kabla ya kwenda kulala, utaufanya mwili wako kuwa vizuri na kulainisha hisia na mifupa yako ya mwili, hii itakufanya ulale vizuri na kuwa na utashi mzuri kwa ajili ya kuamka asubuhi.

Tumeona faida hizi za kushangaza ambazo zinaweza kutokea katika mwili wako utakapoanza kutumia maji ya moto kila asubuhi na jioni .

Anza sasa kutumia maji ya moto kila siku ili uone faida nzuri tulizosoma hapo juu kwa ajili ya manufaa yako .

Mimi nimeanza kujaribu na nimeona kuna faida anza na wewe leo.