NA ABOUD MAHMOUD

MAKOCHA wa mchezo wa soka visiwani Zanzibar wameshauri kuongeza taalamu ya mchezo huo, ili waweze kufika mbali na kupata kufundisha timu za nje.

Akizungumza na Zanzibar Leo, aliekuwa mchezaji wa zamani katika timu mbali mbali ikiwemo ya Taifa, Said Mohammed Said (Kuzu).

Alisema ni vyema makocha wakajiendeleza kielimu ili kufahamu mambo mbali mbali, badala ya kubaki na ufahamu kwa sababu walikuwa wachezaji wa zamani.

Alisema kwamba mwalimu wa soka akiwa na taaluma ya mchezo huo anaweza kufikia malengo aliyokusudia kwani mchezo huo unabadilika siku hadi siku.

“Nawashauri walimu wa soka wasikae na kusema wao wamecheza mpira na kutumia ujuzi ule ule wa zamani,kwa wakati huu tunaokwenda nao lazima tubadilike tupite darasani kujifunza ili kupata elimu zaidi,alisema.

Alisema ni vyema wachezaji wawe na malengo yenye faida na wao ambayo yatawasadia kufika mbali kwa kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.