NA MWAJUMA JUMA

MABANATI wa timu ya Kikapu wa kikosi cha Valantia (KVZ) wametwaa ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja 2020/2021.

KVZ imefanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kumaliza ligi ikiwa na pointi nane, baada ya juzi kupata ushindi wa bure kufuatia wapinzani wao kushindwa kutokea uwanjani.

Mchezo huo ulipangwa kuchezwa juzi katika uwanja wa Mao Zedong  kati ya timu hiyo na African Magic.

Mchezo huo ambao ulipangwa kuchezwa majira ya saa 10:00 za jioni, KVZ ilifika mapema  na kuanza kufanya mazoezi ya kupasha misuli, na ulipofika muda wa kuanza walikaguliwa na  mpaka mwamuzi anamaliza kukaguwa na kusubiria kwa muda wapinzani wao walishindwa kutokea.