LONDON, England
MLINDA mlango wa Arsenal, Bernd Leno afunga pingu za maisha na mpenzi wake, Sophie Christin.

Leno na Sophie wamekuwa wakichumbiana kwa kipindi cha miaka minne sasa baada ya kutangaza hadharani kuhusu uhusiano wao mwaka 2015.
Wawili hao waliidhinisha ndoa yao siku ya Jumatano, katika sherehe adi iliyoandaliwa Dusseldorf.

Wachezaji soka nyota akiwemo Rob Holding walimpongeza mlinda lango huyo Mjerumani kwa kufanya harusi.

Wapenzi hao watakuwa wakifurahia msimu uliobakia pamba kabla ya Bernd kurudi London kwa ajili ya maandalizi ya msimu na Arsenal.

Leno mwenye umri wa miaka 28, alikosa miezi ya mwisho ya msimu kutokana na maumizi na sasa anakaribia kupona.(Goal).