Yanga,Simba kukutana Oktoba 18
NA MWANDISHI WETU
LIGI Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu, mabingwa watetezi, Simba SC wakifungua dimba na Ihefu FC uwanja wa High Land Estate, Mbarali mkoani Mbeya.
Watani wao wa jadi, Yanga SC wataanzia nyumbani, uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya.
Mechi nyingine zote za ufunguzi zitatanguliwa na mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 29 kati ya mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzana (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation (ASFC) Namungo FC na mabingwa wa Lig Kuu Simba SC Jumapili ya saa 11:,00 Uwanja wa Mkapa.
Wenyewe kwa wenyewe, watani wa jadi, Yanga na Simba watakutana Oktoba 18 katika mechi ya mzunguruko wa kwanza wa Ligi Kuu.