NA MWAJUMA JUMA

LIGI Kuu soka Zanzibar ya Wanawake inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 6 mwaka huu.

Ligi hiyo itashirikisha timu tano itachezwa katika uwanja wa Mao Zedong, ina lengo kuziandaa timu hizo kwa ajili ya maandalizi ya ligi ya mwakani.

Katibu wa soka la Wanawake Zanzibar Hawa Abdalla akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema ligi itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Alifahamisha kwamba licha ya kuwa mtindo utakaotumika ni wa nyumbani na ugenini, lakini timu hizo zitatumia uwanja mmoja tu ambao ni wa Mao Zedong.

“Tutatumia uwanja mmoja tu wa Mao Zedong ambao kila timu itakuwa inafanya michezo yake ya nyumbani na ugenini “, alisema.