NA MWAJUMA JUMA

LIGI Kuu ya Zanzibar ya mpira wa Kikapu inazidi kuchanja mbunga katika uwanja wa Mao Zedong , ambapo juzi Usolo ilipokea kichapo cha pointi 70-61 dhidi ya Beit el Ras.

Ushindi wa timu hiyo unaifanya kuvuka nafasi moja kutoka wa sita mpaka saba na kuwashusha Usolo, ambao na wao watakua nafasi ya tano wakiwa na pointi sita pia.

Katika mchezo huo miamba hiyo ilionesha ushindani mkali hasa katika robo ya kwanza, ambayo ilimalizika kwa kupitana kwa pointi moja .

Beit el Ras katika robo hiyo ikipata point 14 na Usolo ikajipatia pointi 13, ambapo hadi mapumziko iliongoza Beit el Ras kwa pointi 21-10.

Robo ya tatu ya mchezo huo ilianza na miamba hiyo kuendelea kushambuliana na ilimalizika kwa Beit El Ras kuongoza kwa pointi 20-17.

Katika robo ya nne ambayo ni ya lala salama Usolo ilionekana kuamka kwa kuishinda Beit el Ras, ambayo waliibuka kwa pointi 25-15 lakini kuongoza kwao hakukuweza kubadilisha matokeo ya mchezo huo kwa wapinzani wao ambao waliondoka na ushindi.

Beit el Ras katika mchezo huo mchezaji wao alipata pointi nyingi za kufunga ni Abdul-Aziz Mohammed ambae alipata point 14 na katika timu ya Usolo ni Salum Bakari ambae alipata point 13.

Ligi hiyo leo itaendelea tena kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha African Magic na Nyuki.