WAPENZI wasomaji wetu leo tena tunaendelea na namna ya kujikinga na kujitibu kwa kutumia vyakula vya kienyeji ambapo kwa makusudi nimewachagulia tunda la tikiti maji.
Tunda hili lina faida lukuki kwa binaadamu, lakini wengi hawafahamu hivyo licha ya upatikanaji wake ni rahisi na kwa bei rahisi.
Tikiti maji lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.
Tunda hili linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.
Faida 13 za tikiti maji kiafya
• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
• Huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume
NB: Tikiti halifai kutumika katika program ya kupunguza uzito/kitambi kutokana na kuwa na sukari nyingi japo ni sukari ya asili, lakini sisi tuna-discouraged sukari zote kwa tatizo la uzito.