LONDON, England
KOCHA Msaidizi wa Arsenal, Freddie Ljungberg, anaondoka klabuni hapo kutafuta fursa mpya.
Katika taarifa yake, Ljungberg alisema amechukua uamuzi wa kuondoka ili kuendeleza uzoefu wake wa usimamizi.


Ljungberg (43), alikuwa katika madaraka ya muda baada ya kuondoka kwa Unai Emery mnamo Novemba 2019 na kubakia kwenye benchi la ufundi baada ya kuteuliwa kwa Mikel Arteta.
Pia alikifundisha kikosi cha Arsenal chini ya umri wa miaka 15 na 23.
Ikiwa mchezaji, Ljungberg alicheza michezo 326 na Arsenal na alikuwa sehemu ya miamba hiyo iliyotwaa ubingwa wa England kwa rekodi msimu wa 2003-04.
“Nimekuwa nikihusika na klabu hii kuendelea nayo tangu 1998 na nashukuru kwa fursa zote walizonipa kama mchezaji na kama kocha”, Ljungberg alisema.
“Nawatakia Mikel na timu yote kila mafanikio kwa msimu ujao. Tunawashukuru pia mashabiki kwa msaada wao wa kila wakati na kwa kuwa karibu nami kila wakati. Natumai tutakutana tena hivi karibuni.”
“Freddie amekuwa mshiriki muhimu wa timu yangu tangu kuwasili kwangu”, alisema, Arteta.
“Alifanya kazi nzuri kuibeba timu wakati Unai alipoondoka na sisi sote tunamuheshimu kwa asilia 100% kama mtu na meneja. Ninajua nitakutana naye kwenye safu ya usoni wakati ujao.”
Mkurugenzi wa ufundi wa Arsenal, Edu, alieleza Ljungberg alikuwa na fursa mbali mbali katika miezi 12 iliyopita na alishikilia kazi katika Arsenal”, na kuongeza: “Sasa ana nafasi ya kuzingatia chaguzi neyengine, na inaeleweka kwa kazi yake wakati huu”.
Ljungberg aliisaidia Arsenal kutwaa ubingwa wa Kombe la FA msimu huu sambamba na meneja, Mikel Arteta. (BBC Sports).