PARIS,UFARANSA

IDADI   iliyofanywa na Shirika la habari la Ufaransa AFP,kutokana na takwimu rasmi zinaonyesha kuwa maambukizi ya virusi vya corona duniani yamepindukia milioni 18.

Hayo yalijiri wakati ambapo kiwango cha maambukizi ya virusi hivyo kinaendelea kuongezeka kwa kasi.

Zaidi ya nusu ya visa vya maambukizi duniani viko nchini Marekani na katika ukanda wa Marekani Kusini na eneo la Caribbean.

Marekani ndiyo nchi iliyoathirika zaidi ikiwa na zaidi ya visa milioni nne na vifo zaidi ya laki moja na nusu.

Brazil ndiyo ya pili ikiwa na karibu visa milioni tatu na zaidi ya vifo 94 elfu.

Kote duniani kumeripotiwa vifo 687,941,idadi hii iliyofikiwa kwa kutumia data za AFP kutoka kwa serikali na taarifa za Shirika la Afya Duniani WHO ,huenda ikawa inaonyesha idadi ndogo tu ya maambukizi kamili.