KAMPALA,UGANDA

KARIBU wawakilishi 37 kutoka Baraza la Maaskofu  wa Kanisa la Uganda walikusanyika huko Ndeeba kutoa pole kwa Wakristo wa Kanisa la St Peter, ambalo nyumba yake ya ibada ilibomolewa.

Wakiongozwa na mkuu wao na Askofu wa Rwenzori Kusini Jackson Nderebende,kwa pamoja maaskofu hao walisema kwamba Jaji nchini Uganda anapaswa kutekeleza jukumu lake kwa uangalifu na kimaadili.

“Usiangalie tu sheria zilizoandikwa,angalia na maadili katika kuharibu jengo la ibada.Shambulio kwa kanisa moja ni sawa na kushambulia makanisa yote ya Anglikana kwani wote ni ndugu”,Askofu Nderebende alisema.

“Unawezaje kukaa kwenye kiti chako na kuhalalisha uharibifu wa kanisa la Mungu? Tunajua kuna nafasi ya mazungumzo na majadiliano.Kwa maoni yangu,ndivyo jaji makini anapaswa kuamua ili suala kama hili lisuluhishwe kwa amani,”alisema.

Alisema uamuzi wa kuvunja kanisa hilo ni aibu kwa nchi na unaitia doa historia ya Uganda.

Mnamo Julai 10, amri ya mwisho ya kubomoa kanisa ilitolewa na kutekelezwa kwa ruhusa kutoka kwa Mamlaka ya Jiji la Kampala, kwa idhini iliyotolewa na kaimu Mpangaji Ivan Katongole.

“Nguvu za waumini kwa pamoja na marafiki pamoja na Serikali ya Uganda, zitarejesha kanisa hili na litakuwa kanisa zuri zaidi kuliko lilivyokuwa awali.Kwa hivyo, tunawaomba watu watulie, “Askofu Nderebende alisema.

Maaskofu wengi, waliomba Serikali kuhakikisha kanisa hilo linajengwa haraka kwa wakati uliopangwa,ambapo walishangazwa kuwa Kanisa lote lilibomolewa lakini msalaba ulibaki umesimama.

Mkurugenzi wa maadili na uadilifu katika ofisi ya Rais, Rev Can Aaron Mwesigye, alisema kuna mkutano uliopangwa kati ya Rais na Askofu mkuu kujadili suala hilo.

“Baraza la Mawaziri litajadili suala hili na kutafuta njia ya kujenga kanisa. Askofu mkuu ametoa miadi ya kukutana na Rais na hii itafanyika hivi karibuni,”alisema.