NA ZAINAB ATUPAE

UONGOZI wa Soka Wilaya ya Maghabibi ’B’ Unguja umekabidhi zawadi kwa timu zilizopata ubingwa na kupanda daraja la pili kwenda Mkoa na la tatu kwenda la pili Wilaya.

Akizungumza mara ya kukabidhi zawadi hizo huko uwanja wa michezo Maungani Katibu wa Soka Wilaya hiyo Omar Abuu,alisema licha ya kuwa na zawadi kidogo,lakini anaamini kuwa zitawasaidia.

Alisema  lengo lao kutoa zawadi nyingi ambazo zingesaidia kwenye usajili wao,lakini kutokana na hali walilazimika kutoa walichokipata.

“Tulitarajia kutoa zawadi nyingi kwa lengo la kuhamasisha vijana wetu,lakini hali imekuwa mbaya”alisema.

Alizitaka timu ambazo zimepata nafasi ya kupanda daraja msimu huu, kujiandaa vyema kwa ajili ya kupambana,huku daraja walilopanda ni gumu zaidi.

Timu zilizopanda daraja kutoka daraja la pili wilaya kwenda Mkoani ni Villa FC ambayo ilipata kombe n 600,000,  kwa upande wa daraja la tatu kwenda la pili wilaya ni  timu ya Manter line ambayo ilijipatia 400,000.

Nyengine ni,Chukwani,New Star na Afrikan Cost ambazo zitakabidhiwa jezi seti moja moja kwa kila timu.

Timu zilizoshuka daraja kutoka la pili wilaya kwenda la tatu ni Chem Mchem na Sanifuu Hambee.