NA MARIA INVIOLATA
“NAAMINI Celine ataweza kufanya kazi vizuri bila kuwa na mimi”, alisema Rene Angelil katika shoo 40 alizotumbuiza mwanamama huyo, kuanzia Agosti 27 hadi Januari 2016 wakati mume wake akipigania maisha yake.
Utabiri huo kwa bingwa wa miondoko ya R&B Marie Claudette Dion umekuwa kweli pale alipoachia albam mpya “Courage” ya kwanza tangu meneja wake na mumewe alipopoteza vita yake na saratani Januari 14, 2016 njia ndefu ya meneja huyo kumfikisha kileleni Celine Dion ikafika mwisho.
“Kiukweli naogopa sana kumpoteza mume wangu!” Ingawa nimemhakikishia kusimama imara pindi atakapoondoka kilinukuliwa chanzo kilichokuwa karibu na Celine wakati mumewe akipigania uhai wake. Alitaka niendelea kuimba baada ya yeye kuondoka,
“Ni kama, wakati siko jukwaani, mashabiki wangu wako nyumbani ninaenda hotelini kwa mfano, sina mazungumzo na mtu.” Mrembo huyo alifichua kuwa anakosa kila kitu kutoka kwa mumewe na meneja wake huyo.
Alipohojiwa na Gayle King katika kipindi cha “This morning” kinachorushwa na televisheni ya CBS kuhusu albamu yake mpya na ya kwanza bila Renne, alianza kwa kuzungumzia maisha yake na Renne.
Alisema harufu yake, mguso wake vilimsababisha acheke, mrembo huyo alifunua yaliyo moyoni mwake kutokana na kuwa na maisha ya kutokuwa na mpenzi wake aliyetengana naye kwa sababu ya kifo.
Albam hiyo iliyopambwa na wimbo “Courage” ina vibao vyengine vikali kama vile “Flying on My Own”, “Lovers Never Die”, “The Chase” na nyingine zinazodhihilisha umahiri wa sauti ya mwanamama huyo anayeelekea uzeeni.
Licha ya uchungu alio nao, Dion alisema yuko tayari kupata mapenzi mwengine mpya”. “Rene atakuwa nami kila siku, lakini sina uchungu, akimaanisha kutomuona kimwili.
Akizungumza kwa kujiamini anavyofanya kazi bila meneja wake yaani Renne na jinsi anavyojielekeza alisema anajiambia hivi: Acha maumivu, Sema ndio. Sema ndio kwa kucheza. Sema ndio kwa urafiki,”, “Sema ndio kwa upendo labda siku moja. Sijui.”
“Je! Uko wazi kwa hilo?” King aliuliza kwa mshangao bila kuamini kama kweli maneno hayo yanatamkwa na na Celine anayemfahamu!.
“Ndio,”. “Nafungua kitabu … niko wazi. Niko tayari? Hapana? Itatokea? Sijui. Lakini sina msisitizo hata kidogo. Ninafurahia maisha yangu ya sasa zaidi kuliko awali”, anajibu.
Awali ET ilipozungumza na Dion mnamo mwezi Septemba mwaka alisisitiza taarifa hizo, na kubainisha kuwa ingawa “hatapata mapenzi kama ya Rene tena hapa duniani lakini anafuraha maishani mwake.
“Nimo katika mapenzi, ninapenda maisha yangu, ninapenda watoto wangu, ninapenda kazi yangu. Ninapenda kile ninachofanya leo hata zaidi kuliko awali.
“Je! Nitakuwa na mwenza mwengine katika maisha yangu? Tuache ilivyo, nikifanya hivyo itakuwa raha kushiriki hilo”,alisema. “Ni sura ambayo imefungwa, lakini sio kitu ambacho kimekufa. Unabadilika na labda wakati mwingine unakutana na rafiki na inabadilika kuwa kitu kikubwa kuliko hicho. Nani anajua labda sivyo? Lakini nitakujulisha. Ninaahidi.”
Mahojiano na CBS yalifanyika siku chache kabla ya mwanamziki huyo huyo kuachia albam yake mpya ya “Courage” inayoambatana na safari ya kwanza ya maonyesho kadhaa tangu kifo cha mumewe na meneja wake Rene Angelil.
Dion anasema “Ilinibidi nijithibitishie mwenyewe kuwa naweza. Nilihitaji kudhibitishia familia yangu, marafiki, wafanyibiashara, tasnia ya muziki, mashabiki … kwamba naweza kuimba na kuendelea na sio kugangaganga tu, lakini ni kazi, “alisema. “Ninahisi kama naweza kufanya chochote ninachotaka. Niko vizuri kila wakati na nitakuwa vizuri wakati wote.”
“Ninapoangalia nyuma, familia yangu imepitia mengi, kumpoteza mume wangu, meneja wangu, baba wa watoto wangu na rafiki yangu,” “Ninahisi mtetemo wake na msaada wake,”alisema.
‘Courage’ ni albamu ya kumi na mbili kwa lugha ya kiingereza ya Celine Dion, iliyofyatuliwa na studio ya Columbia Novemba 15, 2019.
Ni Albamu yake ya kwanza ya Kiingereza katika miaka sita iliyopita baada ya albam ya “Loved Me Back to Life” (2013). Dion amefanya kazi kwa “Ujasiri” mkubwa kama lilivyo jina la albam hiyo yaani “Courage”.
Kazi hiyo imewashirikisha waandishi , maprodyuza wenye uwezo kama vile Sia, David Guetta, Greg Kurstin, Sam Smith, Star Gate, Jimmy Napes, Lauv, LP, Jörgen Elofsson, Stephan Moccio, Eg White, Liz Rodrigues wa ‘The New Royales’, na wengine wengi.
Mama huyo amethibitisha kwa vitendo ilihali akiomboleza kifo cha mumewe na meneja wake nyuma ya pazia akifanya kazi ya uzalishaji, kupanga ziara yake, kitu ambacho Rene Angelil alikuwa amekishughulikia kabla ya kifo chake.
Kwa hakika hiyo ni hatua yake mpya baada ya kuondokewa na kiongozi wa kazi zake na mwandani wake.
“Nimeshughulika sana, sio katika albamu yangu hiyo tu hasa katika utengenezaji na maandalizi ya uzinduzi wa onyesho hili. Nilisema kile ninachokipenda siyo maoni ya shinikizo. Inaweza kuakisi vibaya. Sijui kama ni sawa”. “Ninauliza kusikilizwa,” alisema kimwana huyo kwa ujasiri.

“Sikutaka huko (kabla ya kifo cha Angelil). Sikutaka kuwa kwenye mikutano. Nilitaka tu kuimba kwa njia bora zaidi na ndiyo hiyo … Lakini sasa Rene hayupo hapa” Mbali na kutaka kudhibitisha uwezo wake Dion anasimama tena bila mumewe na meneja wake.
Akithibitisha uwezo wake anasema kuwa muziki wa maonyesho umo ndani ya damu yake! Kitu ambacho Renne na kaka yake walikigundua mapema, ikumbukwe kaka yake Celine, Daniel Dion ndiye aliyemuomba Rene kuendeleza kipaji cha mrembo huyo.
Alisema anaendeleza anachopenda zaidi umekuwa “Utegemezi au Uraibu” kaka yake huyo naye alifariki siku mbili tu baada ya kifo cha mumewe.
Miezi sita baada ya kifo cha mumewe Celine alisema hivi: Tulikuwa nusu kwa nusu
(50/50) – Nadhani aliondoka na asilimia 50 (alipofariki) lakini sasa 50 imerudi tena kwangu, nahisi nguvu sana na kusimama, imerudi tena na kwa watoto wangu, ‘Ni vizuri. ‘
Awali, wakati wa mahojiano na ET Dion alifunguka kwa nini aliamua kutayarisha albamu yake hiyo Courage alisema hivi: “Inawakilisha maisha yake mapya kupitia albamu hiyo katika safari binafsi na kimuziki , njia ya mavazi, kuongea, huwezi kumfurahisha kila mtu,” alisema. “Ninavaa kwa ajili yangu na jinsi ninavyohisi, wazia kuwa kila mtu anapaswa kuhisi hivyo. “
Mahojianao hayo yanayohusu maisha yake kimuziki na binafsi tangu kifo cha mumuwe, yameongeza umaarufu wa mrembo huyo ilihali akiwatia kiwewe mashabiki wake na wapenzi wa tasnia ya muziki wakisubiri kwa hamu juu ya nani atakayejaliwa kutoka na kimwana huyo anayesemekana mumewe na meneja wake yaani Rene ndiye pekee aliyeonja penzi la kimwana huyo.
Rene Angelil, aliyekuwa mume wa mwanamuziki Celine Dion, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73 na walifunga ndoa mwaka 1994 na wakajaliwa watoto watatu.
Rene Angelil alifariki Las Vegas baada ya kuugua saratani wakati mumewe akiugua Dion alichukua likizo kutoka kwenye muziki kwa vipindi viwili ili kumtunza Angelil baada yake kupatikana na saratani ya koo mwaka 2000.
Angelil alizaliwa mjini Montreal mwaka 1942. Baada ya kuwa meneja wa makundi kadha nchini Canada, aliombwa na wazazi wa Dion awe meneja wake mwanamuziki huyo alipokuwa na umri wa miaka 12 tu.
Gazeti la Montreal Gazette liliwahi kuandika kwamba Angelil aliweka rehani nyumba yake ili kupata pesa za kufadhili albamu ya kwanza ya mwanamuziki huyo.
Dion amerekodi albamu 25 studioni na ndiye mwanamuziki wa tano kwa kulipwa pesa nyingi zaidi, utajiri duniani akikisiwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 630.
Mwaka 1999, wimbo wake My Heart Will Go On, uliotumiwa katika filamu ya Titanic, ulishinda tuzo mbili za Grammy.