LONDON, England

GABRIEL JESUS aliiongoza timu yake ya Manchester City kwa kuwafungia wenyeji,bao la ushindi dakika ya 68 ikiwalaza Real Madrid ya Hispania 2-1.

Katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia jana Uwanja wa Etihad.

Raheem Sterling alianza kuifungia Man City dakika ya tisa kwa pasi ya Gabriel Jesus, kabla ya Karim Benzema kuisawazishia Real dakika ya 28.

Kwa matokeo hayo kikosi cha Pep Guardiola kinakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia awali kushinda 2-1, pia kwenye mchezo wa kwanza Madrid na nayo  Olympique Lyon ya Ufaransa iliitoa Juventus ya Italia.