WASHINGTON,MAREKANI

MAREKANI imerikodi zaidi ya vifo 2,000 kutokana na ugonjwa wa COVID-19 katika muda wa masaa 24, ikiwa ni idadi ya juu kabisa ya vifo katika muda wa miezi mitatu.

Takwimu  hizo ni kwa mujibu wa chuo kikuu cha Johns Hopkins kama kilivyoeleza Nchi hiyo, ambayo ilishuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya corona tangu mwishoni mwa mwezi Juni.

Ilielezwa kuwa idadi ya vifo 2,060 kwa siku moja pamoja na zaidi ya maambukizi mapya yanayofikia watu 58,000, chuo hicho kikuu kilichoko mjini Baltimore .

Mara ya mwisho Marekani kurikodi zaidi ya vifo 2,000 katika muda wa masaa 24 ilikuwa Mei 7.

Idadi ya watu waliofariki nchini Mexico ilipindukia 50,000 Serikali ilisema, ikiwa ni siku chache tu baada ya kuwa nchi ya tatu yenye vifo vingi duniani.

Wizara ya afya ilitangaza vifo zaidi 819 katika taarifa yake ya kila siku na kufikisha jumla ya vifo 50,517 tangu taifa hilo la Marekani kusini kutangaza kesi ya kwanza mwezi Februari mwaka huu.