KIGALI, RWANDA

RWANDA imeyafungia masoko mawili ya Nyabugogo na Soko la jiji la Nyarugenge kuanzia jana kwa muda wa wiki moja ili kudhibiti maambukizi mapya ya corona huko Kigali.

Uamuzi huo unakuja baada ya Serikali kusema kuwa watu 253 ambao walipimwa Covid-19 nchini wengi walitoka masoko ya Nyarugenge na Nyabugogo pamoja na wachache kutoka maeneo mengine.Kati ya kesi hizo zilizogunduliwa jiji la Kigali pekee lina kesi 219

Meya wa Jiji la Kigali, Pudence Rubingisa alisema kwamba wale wanaofanya kazi katika soko hilo,haswa wale wanaouza watapewa muda wa kuondoa hisa zao na kuhamia katika soko jengine.

Mtangazaji wa kitaifa,Rubingisa alisema kwamba kuna mtazamo mbaya wa  kufuata miongozo rahisi inayohitaji mtu kuosha mikono mara kwa mara, kuvaa  barakoa na kukaa mbali baina ya mtu na mtu.

Rubingisa alisema Jiji la Kigali lina idadi kubwa ya watu na juhudi zilizowekwa katika kutekeleza miongozo ya usalama ya Covid-19 bado hazitekelezwi ipasavyo.

Waziri wa Afya Dkt.Daniel Ngamije alisema kuwa vipimo ndani ya masoko yote ya Kigali na maeneo mengine yenye hatari kubwa vitafanywa wiki hii ili kuamua hatua za kufuata au kuongeza vizuizi vyengine.

“Kuzuia shughuli ni uamuzi mgumu lakini unawezekana Watu wanahitaji kujua kwamba ikiwa idadi itaendelea kuongezeka, kuna maamuzi kadhaa magumu ambayo italazimika kufanywa.Wiki hii tunafanya vipimo katika masoko yote ya Jiji la Kigali na matokeo yake ndio yatakayoamua hatua nyengine za kuchukua,”alisema.

Msemaji wa polisi CP John Bosco Kabera alisema kuwa hatua za kujikinga na Covid-19 zinapaswa kuwa tofauti sasa kama ilivyokuwa mwanzo kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya watu.