MILAN, Italia
KLABU ya Inter Miami imekamilisha kumsaini kiungo, Blaise Matuidi, akiwa jina kubwa la kwanza kusajiliwa na miamba hiyo ya Ligi Kuu ya Marekani.
Matuidi na mabingwa wa Italia, Juventus walikubaliana kumaliza mkataba wa mwaka mmoja wa mwisho siku ya Jumatano.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa mwenye umri wa miaka 33, alicheza na mmiliki mwenza wa Inter Miami, David Beckham huko Paris St-Germain kabla ya kujiunga na Juve mnamo 2017.
“Natumai tutashinda mataji mengi pamoja,” alisema, Matuidi. “Ni changamoto kubwa kwangu.”
Inter Miami wamepoteza mechi zote tano hadi sasa kwenye msimu wao wa kwanza wa MLS, ambao ulianza tena Agosti 22.
“Sikuweza kuwa mwenye furaha zaidi kumkaribisha rafiki yangu Blaise kwa Inter Miami,” alisema Beckham, kiungo wa zamani wa England na Manchester United.(Goal).