NAIROBI, Kenya

MBIO za kimataifa za Kip Keino Classic zilizokuwa ziandaliwe katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo, Nairobi mnamo Septemba 26, 2020, sasa zimeahirishwa hadi Oktoba 3, 2020.

 Kubadilishwa kwa ratiba ya mbio hizo kunachochewa na mabadiliko kwenye ratiba ya mashindano mbalimbali ya riadha.

Riadha za Kip Keino Classic sasa zitaandaliwa siku moja kabla ya Mkenya Eliud Kipchoge na Kenenisa Bekele wa Ethiopia kunogesha mbio za London Marathon.

 Kip Keino Classic ni miongoni mwa mbizo za  kivumbi cha World Athletics Continental Tour kilichofunguliwa rasmi jijini Turku, Finland mnamo Agosti 11, 2020.