ZASPOTI
MABINGWA wa Belarus, Minsk wamepata huduma za mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroun, Henriette Akaba kwa msimu uliobakia 2020.


Akaba amefanya uhamisho wake kwenda kwa vigogo wa Belarus akitokea klabu ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Cameroun, Amazone FAP baada ya kufanyiwa vipimo vya matibabu na kukubali maslahi kibinafsi na timu ya Volodymyr Reva.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliwahi kukipiga na Trabzon Idmanocagi ya Uturuki, Energy Voronezh ya Russia, Bangkokthonburi ya Thailand na Besiktas kwa muda mfupi mnamo 2018.


Kwenye hatua ya kimataifa, anaonekana mara tano kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika la Wanawake, fainali mbili za Kombe la Dunia za Wanawake wakubwa wakati akicheza mara 34 akiwa Indomitable Lionesses. (Goal).