BARCELONA, Hispania
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi, ameifahamisha rasmi klabu yake kuwa anataka kuondoka msimu huu wa kiangazi.

Habari hiyo nzito imekuja kama bomu kwa kocha mpya, Ronald Koeman na uongozi wa Barca na kuwatumbukiza miamba hiyo katika matatizo zaidi.

Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 33, alituma ujumbe wa ‘Fax’ kwa klabu siku ya Jumanne akisema anatamani kuondoka kwa uhuru mara moja.

Barca ilitandikwa magoli 8-2 na Bayern Munich katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hivi karibuni.
Mshindi huyo wa mara sita wa tuzo ya ‘Ballon d’Or’ alianza kuichezea Barca mwaka 2004 na kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne akiichezea klabu hiyo.

Barcelona inaamini kifungu cha mkataba cha kumruhusu kuondoka kimekwisha na mkataba wake unakwisha mwaka 2021 na kifungu cha kumuuza cha pauni milioni 700.

Bodi ya klabu hiyo itakaa hivi karibuni na wengine wanaona kuwa jambo pekee ambalo linaweza kubadili nia ya Messi ni kujiuzulu kwa rais Josep Maria Bartomeu, na uchaguzi ufanyike mapema. Lakini Messi anaonekana kuwa amedhamiria kuondoka klabuni hapo bila ya kujali chochote.

Baada ya taarifa hiyo, mashabiki wa Barca walikusanyika nje ya Nou Camp dhidi ya bodi na wakionesha kumuunga mkono mchezaji huyo aliyeweka rekodi nzuri ya ufungaji.

Mapambano ya kisheria sasa yatakuwa kati ya klabu na mchezaji. Messi alikuwa na kifungu cha mkataba wake kinachomruhusu kuondoka kwa uhuru, ikiwa ataijulisha klabu shauku yake kabla ya tarehe 10 mwezi Juni.

Tarehe hiyo imepita, sasa Barca inaamini kuwa kifungu hicho kimekwisha muda wake, lakini, Messi na timu inaamini kuwa kifungu hicho kinaweza kuongezewa muda mpaka mwezi Agosti kwa sababu ya kipindi cha janga la virusi vya ‘corona’.

Mchezaji mwenzake wa zamani, Carles Puyol, ameandika kwenye ukurasa wake wa ‘twitter’ akimuunga mkono kwa hatua aliyoichukua.
Barcelona wamesema kuwa kifungu hicho kilikwisha tangu tarehe 10 mwezi Juni na kuwa wanashawishika, kuwa watashinda mgogoro huo wa kisheria, kuhusu suala hilo.

Lakini wanasheria wameiambia klabu kuwa Messi hatashinda mgogoro huo.
Ujumbe wa ‘fax’ ni jambo ambalo limefikiriwa vyema, kwa kuwa amezungumza na familia na wanasheria, ana shauku kubwa kuondoka kwenye klabu hiyo. Kwa Messi haya si mapambano ya mamlaka. Anachotaka ni kuondoka tu basi.

Nguvu ya Messi Barcelona.

Messi

Mashabiki wanasema kuwa ana mamlaka makubwa kwenye klabu, huzungumza moja kwa moja ikiwa atatakiwa kufanya hivyo kama ilivyo kwa wachezaji wengine nguli kwenye klabu kubwa.

‘Ni mchezaji mzuri ambaye sijawahi kumuona mwenzake, kocha Pep Guardiola alikuwa na Messi akiwa Barcelona.
Kurejea kwa Neymar, ambako hakukufanyika, kuendelea kwa kocha Ernesto Valverde, ambako hakukufanyika; hakuna haja ya kumsajili Antoine Griezmann, ambako hakukufanyika, hivyo sina uhakika kama ana mamlaka makubwa.

Ni hali ya kuwa hivi sasa Messi hafurahii kuichezea Barca tena, timu ambayo kwa sasa inahitaji kufanya kazi kubwa kushinda mataji makubwa tena. Anataka kuona Barcelona itafanya nini, lakini, huenda pia hatahudhuria mazoezi.Hatafanya vipimo pengine kabla ya msimu. Ikiwa itakuwa hivyo, klabu hiyo itatuma ujumbe wa ‘fax’ kwa Messi kuhusu kutoheshimu mkataba wake na mgogoro wa kisheria ndipo utakapoanzia na huo utawafikisha katika mahakama ya kimichezo hatimaye.

Messi anataka kuondoka sasa hivi bila kujali chochote. Lakini je ataweza? Ukizingatia mkataba wake ulipaswa kuwa kifungu kilipaswa kufanyiwa kazi tarehe 10 mwezi Juni, klabu inaamini kuwa iko kwenye njia sahihi.

Lakini, wanataka kuendelea kubaki na mchezaji ambaye hataki kubaki kllabuni ? Kilabu kama Paris-St Germain na Manchester City zilisisitiza hazijachukua hatua yoyote kuhusu kumnasa Messi. Lakini ni wazi hakuna ajuaye athari za kifedha za hatua hiyo.

Klabu nyengine kubwa zilichukua hata mara nyingi huko nyuma kujaribu kumshawishi Messi kujiunga na timu hizo, Inter Milan na Chelsea.
Shinikizo pekee dhidi ya bodi linatoka kwenye mitandao ya kijamii kama nguvu hiyo inamlazimu Bartomeu kujiuzulu.

Klabu pengine itamtaka aendelee kubakia lakini, anaweza akalazimika kujadili kuhusu ada kubwa ya uhamisho. Hivyo kama Barcelona kweli wataamua kuomba kiasi hicho kikubwa zaidi cha fedha au nani yuko tayari kulipa ada ya uhamisho. Ingawa amesaliwa na mwaka mmoja tu wa mkataba wake, mzozo huu utaendelea kwa muda.(BBC Sports).