CARACAS, VENEZUELA

MEYA wa mji mkuu wa Venezuela Caracas, Dario Vivas, amefariki hapo juzi  Alhamisi akiwa na umri wa miaka 70 baada ya kuugua COVID-19 kwa zaidi ya wiki tatu.

Vivas alitangaza mnamo Julai 18 kuwa alikuwa amepima virusi vya COVID-19 na alikuwa akifatiwa matibabu akiwa peke yake.

“Ninaripoti kuwa na … COVID-19,” Vivas alisema kwenye mtandao wakati huo.

Maafisa wengine wa Venezuela ambao walijpatikana kuwa na COVID-19 ni pamoja na Diosdado Cabello, rais wa Bunge la Jimbo Kuu (ANC), ambaye alitolewa hospitalini hivi karibuni; Waziri wa Mafuta Tareck El Aissami, na magavana na meya kadhaa wa taifa hilo la Amerika Kusini.

Vivas aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Capital mnamo Januari.