KIGALI, RWANDA

RWANDA imezindua mfumo wa usajili wa raia ambao umekuwa na wasiwasi kwamba wakimbizi,wakaazi wa kigeni na raia wanaoishi nje ya nchi hawakujumuishwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utambulisho la Kitaifa Josephine Mukesha, alisema mfumo huo hautomuacha mtu yoyote katika usajili huo.

“Kila mtu wakiwemo wakimbizi,wakaazi wa kigeni pamoja na Wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi,”aliliambia New Times.

Mfumo wa usajili wa kuzaliwa na vifo ulizinduliwa Agosti 10,2020.

Rwanda ilisisitiza juu ya umuhimu wa kumfanya kila mtu aonekane kupitia mfumo wa usajili mzuri wa raia na mfumo wa takwimu muhimu katika Hospitali zote zinazokusanya idadi ya watu na matukio yote yanayotokea nchini.

“Sio kwa Warwanda tu tunafanya kazi na Wizara ya usimamizi wa dharura na UNHCR tunaungana na mifumo yao ili warudishe data kwenye mifumo yao mara tu matukio haya mawili ya kuzaliwa na vifo yatakaporikodiwa,”Mukesha alisema.

Mukesha alisema wanashirikiana na shirika la umoja wa Mataifa kwa sababu rikodi za wakimbizi zinashughulikiwa na chombo cha UN.

Takwimu za shirika la UN la wakimbizi zinaonyesha kuwa Rwanda hivi sasa ina wakimbizi 149,149 na wanaotafuta hifadhi 76,853 kutoka DR Congo.Rwanda pia ina wakimbizi wenyeji 71,973 kutoka Burundi.

Maendeleo hayo yanakuja baada ya sheria juu ya Watu na familia kurekebishwa mnamo 2 Februari kuongeza haki za msajili wa umma kwa vituo vya afya kusajili vizazi na vifo vinavyotokea katika vituo vya afya na jamii.

Amri zinazohusiana na mawaziri zilizochapishwa kwenye gazeti la kitaifa la Julai 27, zilibaini wafanyakazi wa kituo cha afya ambao watapewa majukumu ya msajili wa raia kulingana na aina ya kituo cha afya.

Awamu ya kwanza katika uzinduzi huo ni pamoja na Hospitali zote nchini Rwanda ambazo ni 56 katika Wilaya zote.

Mfumo huo mpya utatekelezwa hatua kwa hatua katika vituo vyote vya afya vilivyobaki.

Kuna vituo vya afya 550 pamoja na vya kibinafsi na katika kila kituo cha afya wafanyakazi wawili walipata mafunzo, moja ikiwa meneja wa data na mwengine msajili wa raia.

Mkurugenzi wa kitengo cha wauguzi na wakunga au mkuu wa kituo cha afya au mkurugenzi wa kituo cha afya cha kibinafsi atapewa haki ya kufanys kama msajili wa raia kusajili hafla za kuzaliwa na vifo kulingana na aina ya kituo cha afya.

Usajili wa raia ni rikodi ya kuendelea ya kudumu, ya lazima na ya ulimwengu na sifa za matukio muhimu,kama kuzaliwa na kifo, ya idadi ya watu kwa mujibu wa sheria.

Kiwango cha usajili nchini  bado kiko chini kuliko lengo la kimataifa la asilimia 90 ifikapo 2025, kitu ambacho Serikali inafanya kazi kubadili haraka sana.

Usajili wa kifo pia unasimama kwa asilimia 30,Rwanda inataka kuongeza usajili wa kuzaliwa na kifo na udhibitisho kwa asilimia 95 na asilimia 90, dhidi ya malengo ya kimataifa ya asilimia 90 na 70, ifikapo 2025.