MICHELLE Obama ni mke wa aliyekuwa rais wa Marekani, Barack Obama ambaye ni rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuliongoza taifa hilo kubwa kwa vipindi viwili vya jumla ya miaka minane.

Kwa sababu alikuwa mke wa rais, Michelle Obama akachukua nafasi ya kuwa mama wa kwanza mweusi wa taifa la Marekani na mnamo mwaka 2018, Michelle alitajwa kama mmoja wa wanawake anayependwa zaidi nchini Marekani.

Kwa mujibu wa kampuni ya utafiti wa kimataifa, Gallup, ilieleza kwamba sifa hiyo ya mwanamke mwenye kupendwa zaidi nchini Marekani alikuwa nayo Hillary Clinton kwa muda wa miaka 17, ahata hivyo mnamo mwaka 2018 Michelle akachukua nafasi hiyo.

Kwa kawaida Michelle Obama ni mmoja kati ya wanawake wapole na ni nadra sana kuzungumza, hata hivyo anapozungumza huwa kuna kitu muhimu ambacho kinamlazimu akiseme.

Wakati huu akiwa mumewe amestaafu urais wa Marekani, Michelle amekuwa kimya sana, hata hivyo hivi karibuni alilazimika kuzungumza kwa lengo la kuweka sawa mustakabali wa siasa za taifa hilo.

Katika hali ambayo hauikutarajiwa Michelle Obama amemshambulia kwa maneno makali rais wa Marekani Donald Trump kwenye mmoja ya hafla za mikutano ya kampeni za urais kupitia chama cha democratic.

Michelle ambaye amesimama kumpigia kampeni mgombea wa chama cha democratic, Joe Biden kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu, alisema Trump ni mtu sahihi kwa wamarekani kumpa nafasi ya kuwaongoza.

Michellen na Joe Biden

“Donald Trump sio rais sahihi kwa nchi yetu,” amesema aliyekuwa mama taifa wa Marekani katika ujumbe wake wenye hisia uliorekodiwa wakati wa mkutano chama cha democratic.

Waasi wa chama cha Trump cha Republican pia nao hawakusita kutoa yaliyo moyoni wakati wa mkutano huo. Kwa sasa Trump yuko nyuma ya Biden katika kura ya maoni kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.

Kwasababu ya mlipuko wa virusi vya corona, democrats ilifutilia mbali mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika na shughuli nyengine zote za kisiasa huko, Milwaukee, Wisconsin.

Lakini bado hijafahamika ikiwa mikutano hiyo kwa njia ya mtandao ambayo hotuba zake zimerekodiwa na bila uwepo wa watu wanaoshuhudia moja kwa moja kunaweza kusababisha msisimko ule ule kama ya wakati wa kabla ya janga la corona.

Chama cha Republican kitakumbana na changamoto hiyo hiyo wakati wanathibitishia umma umuhimu wao wa kuwa uongozini katika kipindi cha miaka minne kwenye mkutano wao uliopangwa kufanyika wiki ijayo.

Michelle Obama alitumia hafla hiyo kwneye hoatuba yake iliyokuwa   imerekodiwa kabla ya Biden kutangaza mgombea mwenza, seneta Kamala Harris, alimshambulia Trump kwa maneno.

“Huwezi kudanganya mienendo yako unapofanya kazi,” alisema hivyo kwenye hotuba yake ambayo ilifunga siku ya kwanza ya mkutano wa chama cha democrats.

Msemaji huyo mkuu wa siku aliongeza: “Uchumi wetu unadidimia kwasababu ya virusi vya corona hali ambayo imetokana na rais huyo alivyopuuza kwa muda mrefu mrefu kuchukua tahadhari za kukabiliana na ugonjwa huo”.

“Kusema ukweli ulio wazi kwamba maisha ya mtu mweusi ni muhimu bado ni jambo linalofanyiwa dhihaka katika ofisi ya juu”, Michelle aliendelea kusema.

“Kwasababu kila tunapogeukia ikulu kwa uongozi, au kutaka kupata faraja, au kupata nguvu ya uimara, badala yake tunachopata ni ghasia, mgawanyiko na ukosefu wa uelewa kabisa.”

Alisema miaka minne iliyopita imekuwa na changamoto nyingi sana kujieleza kwa watoto wa Marekani. “Wanaona viongozi wetu wakiita wengine maadui wa serikali na kuhamasisha dhana ya kuwa mtu mweupe ni bora”. alisema.

“Wanaangalia kwa hofu wakati watoto wanapotenganishwa na familia wanapotupwa kizimbani, kurushiwa maji ya kuwasha na mabomu ya rashasha yanatumiwa katika maandamano ya amani kwasababu tu ya nafasi ya kutaka kupiga picha.”

Michelle aliendelea kusema, “Donald Trump si rais stahiki kwa nchi yetu. Amekuwa na wakati mwingi sana kujidhihirisha kwamba anaweza kufanya kazi hii, lakini ni wazi kwamba mambo yamemzidi unga.

“Hawezi kuwa yule mtu ambaye sisi tunamtaka awe kwa ajili yetu.”Hivyo ndivyo ilivyo.”

Alimulezea Biden kama “mtu mwenye heshima”, na kuzungumzia uzoefu wa mgombea wa chama cha democratic akiwa makamu wa rais chini ya utawala wa mume wake, Rais Barack Obama.

“Hatuna budi zaidi ya kumpigia kura Joe Biden kama vile maisha yetu yanavyotegemea hilo,” alisema hivyo akiwa amevalia mkufu ulioandikwa “Piga kura”.

Kwa mujibu wa uchambuzi uliotolewa na Anthony Zurcher, wanasiasa wengine wengi wamezungumza katika mkutano wa democratic.  Hata hivyo, aliyejitokeza kuwa na hotuba ya nguvu yenye kugusa hisia za watu ni Michelle Obama pekee.

Katika uchambuzi huo, Zucher alisema ukweli aliosema Michelle ni kwamba Donald Trump hawezi kuwa mtu anayehitajika kuiongoza nchi ya Marekani kwa sasa.

“Hivyo ndivyo ilivyo,” alisema, akirejea maneno yale yale yaliyosemwa na rais hivi karibuni kuhusu kuongezeka kwa idadi ya waliokufa kwa virusi vya corona.

Hakuwa anajaribu kushawishi Rupublicans kuunga mkono upande mwingine. Hiyo ilikuwa ni kazi ya John Kasich.

Hakuwa anajaribu kushawishi watu wa mrengo wa kushoto kumuunga mkono Biden. Bernie Sanders alitatua hilo.

Michelle alikuwa akizunguza na wanachama wa democrats waaminifu, baadhi yao pengine hata wasilia majumbani, au alipigia kura chama pinzani 2016, au baadhi yao huenda ikawa mwaka huu wamekosa imani ama wameingiwa na hofu.

Lengo lake lilikuwa ni kufikisha ujumbe thabiti wenye mvuto na kutoa wito wa kuchukua hatua.