NA MWAJUMA JUMA

UONGOZI wa klabu ya soka ya Mlandege umesema baada ya kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa, wanakusudia kutaka kuonana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, kumkabidhi kombe hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Rais wa Mlandege, Mbaraka Himid,  alisema, kukutana kwao na rais watakuwa na malengo makuu manne ikiwa pamoja na kumtunukia jezi ya timu yao, ikiwa na shukrani yao kwa jitihada zake za kuinua sekta ya michezo nchini.

Alisema, baada ya Mlandege kurudisha historia ya timu za uraiani kuchukua kombe hilo baada ya kipindi cha zaidi ya miaka mitano kutoka Vikosi vya SMZ, litakuwa jambo la faraja kwao kutoa heshima hiyo kwa Dk.Shein.

“Tunataka kuonana na rais ili kumpelekea kombe na kumkabidhi jezi yetu kama ni ishara ya kumuaga”,  alisema.