NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KIUNGO mpya wa klabu ya Simba Bernard  Morrison ambaye alisajiliwa akitokea Yanga, ameomba mashabiki wasimchukia kwani ni kawaida kwa mchezaji kutoka timu moja  kwenda nyingine.

Morrison kabla ya kusajiliwa Simba kulikuwa na changamoto ya kimkataba kati yake na mabosi wake wa zamani Yanga .

Akizungumza na vyombo vya habari mchezaji huyo alisema kutoka Yanga na kwenda Simba kwake ni jambo la kawaida, kama wanavyofanya wachezaji wengine.

Alisema kwenye miasha ya soka mara nyingi jambo hilo hufanyika, hivyo mashabiki wajaribu kumuelewa na kumpokea kama mchezaji wao na wasimchukie.