NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Azam FC Mbaraka Yusuph amesema bado hajajua muelekeo wake kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Mbaraka amemaliza mkataba wake na Azam mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Katika msimu huo mchezaji huyo hakupata nafasi ya kung’ara sana kutokana nakuwa majeruhi ambayo yalikuwa yanamsumbua kwa muda mrefu .

Akizungumza na Zanzibar Leo hivi karibuni Mbaraka alisema amemaliza mkataba wake na Azam, hivyo anaona kama hawana mpango wakumuongezea mkataba.

Alisema anasema hivyo kwani hajajua hatma yake hawaja zungumza naye kwamba watamihitaji tena au vipi.

 “Nimemaliza mkataba wangu na Azam nawasubiria kujua hatma yangu,”alisema

Wakati huohuo mtendaji mkuu wa klabu hiyo Abdulkarim Amin ‘Poppat’ alisema mchezaji huyo walimalizana nae tangu mwezi wa sita hawapo nae.